Pages

Ads 468x60px

Tuesday, May 26, 2015

Rais Kikwete Ateua Mkuu wa Wilaya mmoja, ahamisha Wengine 10



RAIS Jakaya Kikwete amemteua Anthony Mavunde kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa, mkoa wa Dodoma.
 
Aidha, Rais Kikwete amefanya uhamisho wa wakuu 10 wa Wilaya kwa nia ya kuongeza ufanisi katika uongozi wa wilaya mbalimbali nchini.
 
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu kwa vyombo vya habari, katika mabadiliko hayo, Kikwete amemhamisha Luteni Edward ole Lenga kutoka Mkalama, mkoani Singida kwenda wilaya mpya ya Kyerwa, mkoani Kagera.
 
Luteni Lenga anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Luteni Kanali Benedict Kitenga aliyefariki dunia Aprili 20, mwaka huu.
 
Wakuu wengine wa Wilaya ambao Rais Kikwete amewahamisha ni Elizabeth `Betty’ Mkwasa kutoka wilaya ya Dodoma kwenda Mvomero mkoani Morogoro na nafasi yake inachukuliwa na Dk Jasmine Tisike anayetoka Mpwapwa.
 
Agnes Hokororo amehamishwa kutoka Namtumbo mkoani Ruvuma kwenda Tunduru, pia mkoani humo huku Fadhili Nkurlu amehamishwa kutoka Misenyi mkoani Kagera kwenda Mkalama.
 
Wengine ni Chande Nalicho anayehamishwa Tunduru kwenda Namtumbo, Festo Kiswaga kutoka Mvomero kwenda Misenyi, Darry Rwegasira kutoka Karagwe mkoani Kagera kwenda Biharamulo mkoani humo, Elias Tarimo kutoka Biharamulo kwenda Chunya mkoani Mbeya na Deodatus Kinawiro kutoka Chunya kwenda Karagwe.

0 comments:

Post a Comment

SHARE