Pages

Ads 468x60px

Friday, June 12, 2015

Serikali Yatoa Maelekezo Kwa Wenye Magari Mabovu Barabarani



WAMILIKI wa magari wametakiwa kufuata sheria ya kuyaondoa barabarani magari yao  yanayopata ajali ndani ya saa sita.
 
Kauli hiyo ilitolewa bungeni jana na Naibu Waziri wa Ujenzi, Gerson Lwenge wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Al-Shaymaa Kwegyir (CCM).
 
Katika swali lake, Kwegyir alitaka Serikali kutunga sheria ya
kuwawajibisha wamiliki wa magari yanayopata ajali kulipa gharama za kunyanyua magari yao badala ya kuwatumia askari wa usalama barabarani.

Mbunge huyo pia  alitaka kujua kama ipo bei elekezi inayotumika kuwaongoza wamiliki wa winchi kwa kazi ya unyanyuaji wa magari yanayopata ajali.
 
Lwenge alisema  gari linapopta ajali ni wajibu wa mmiliki kuhakikisha anaondoa gari lake mapema iwezekanavyo  ili  kutokuwa na kizuizi cha kufunga barabara.
 
Alisema Sheria ya Barabara namba 13 ya mwaka 2007 inaeleza kuwa gari lolote linaloharibika barabarani linatakiwa kuondolewa na mmiliki.
 
“Hakuna bei elekezi ya kuwaongoza wamiliki  wa winchi kwa kazi ya unyanyuaji wa magari yaliyopata ajali bali kinachofanyika ni maelewano kati ya mwenye winchi na mmliki wa gari lililopata ajali,” alisema.
 
Alisema   sheria hiyo  inaeleza wazi kuwa endapo wamiliki wa magari yanayopata ajali barabarani watachelewa kuita winchi la kuoliondoa gari ndani ya barabara, mamlaka ya barabara italiondoa gari hilo na wamiliki wanawajibika kulipa gharama zilizotumika.
 
Lwenge alisema mbali na kulipa gharama hizo pia mmiliki atatakiwa kulipa faini zitakazoamuliwa kwa mujibu wa Sheria ya Barabara.

0 comments:

Post a Comment

SHARE