Pages

Ads 468x60px

Thursday, May 28, 2015

Urais 2015 kumekucha CCM: Makongoro Nyerere naye kutangaza nia Butiama



Mtoto wa aliyekuwa Rais wa Kwanza wa Tanzania ambaye pia ni baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere ajulikanaye kama Makongoro Nyerere naye anatarajia kutangaza nia ya kugombea urais katika uchaguzi mkuu ujao mwaka 2015.
 
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo  kwa vyombo vya habari imebainisha kuwa Makongoro Nyerere atatangaza nia ya kugombea urais kupitia chama cha Mapinduzi ifikapo tarehe moja mwezi wa sita mwaka  huu  yaani  siku  ya  jumatatu.
 
Makongoro nyerere ameungana  na Waziri  Prof. Mark Mwandosya ambaye naye anatarajia  kutangaza nia siku ya jumatatu huku waziri mkuu wa zamani Edward Lowassa akitangaza kutangaza nia siku ya jumamosi ambayo ni mei 30 mkoani Arusha.

0 comments:

Post a Comment

SHARE