Mshiriki wa Big Brother Afrika ‘BBA’ Hot Shot
2014 kutoka nchini Namibia, Luis Munana,
amemwagia sifa aliyekuwa Miss Tanzania 2016,
Wema Sepetu kuwa ni mwenye mvuto wa
kipekee.
Lakini licha ya kutoa sifa hizo, mshiriki
mwenzao ambaye ndiye mwenyeji wao, Idris
Sultan, hakutokea katika sherehe hiyo jambo
lililozua minong’ono kwa watu baada ya tetesi
kwamba ana ugomvi na Wema Sepetu.
Wema alimwagiwa sifa hizo alipokuwa katika
sherehe za Instagram Party katika viwanja vya
Posta Kijitonyama jijini Dar es Salaam.
“Wasanii ninaowakubali kutoka Tanzania ni
Wema Sepetu, ni mrembo sana nampenda,
wasanii wengine ambao nawakubali ni Shilole,
Ommy Dimpoz pamoja na wimbo wake wa
Wanjera,” alisema.
Washiriki wengine wa BBA waliohudhuria
sherehe hizo ni Nhalanhla na Samantha wote
kutoka nchini Afrika Kusini.
Wasanii wa Tanzania waliohudhuria sherehe
hiyo ni Ben Paul, Izzo Bizness, Shelta, King
Majuto, Stan Bakora, JJ Band, huku
mshereheshaji akiwa Adam Mchomvu, B Dozen
na DJ Ommy.
Hata hivyo, Wema alishukuru kupendwa na
Luis. “Jamanii sina hata la kusema jinsi
ulivyonisifia, nashukuru sana sana,” alijinadi
Wema akishukuru.

Mtanzania
0 comments:
Post a Comment