WAKAZI
 wa Mtaa wa Sechelela Kata ya Tambukareli Chadulu (A) Dodoma wanaotumia 
 dawa za kufubaza makali ya Virusi vya Ukimwi (ARV), wametakiwa kuepuka 
matumizi ya unywaji wa pombe, uvutaji wa sigara na ngono uzembe.
Rai
 hiyo ilitolewa jana na Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Sechelela, 
Robarnt Pangaselo, alipokuwa akizungumza kwa niaba ya wanafunzi hao 
kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika mtaa huo.
Alisema
 utumiaji wa dawa hizo  na unywaji wa pombe, ngono zembe pamoja na 
uvutaji wa sigara unachangia kwa kiasi kikubwa kupunguza nguvu za dawa 
hivyo kuwataka wakazi wa eneo hilo wanaojihusisha na unywaji wa pombe 
hasa kwa wale wanaotumia dawa hizo kujiepusha.
“Changamoto 
 tunayokubaliana nayo ni matumizi sahihi ya dawa za ARV kwani kuna wale 
ambao wamekuwa wakitumia dawa huku wakiwa wanakunywa pombe, wanavuta 
sigara pamoja na ngono zembe, niwaombe wakazi kuachana na jambo hili, 
tuendelee kuzitumia kwa kufuata masharti,” alisema
Hata
 hivyo akizungumza kwenye mkutano huo mwenyekiti huyo alisema kuwa 
katika mtaa huo wanakabiliwa na changamoto ya uchakavu wa majengo  ya 
shule ya Medeli    kutokana na uchakavu uliopo hali inayosababisha 
hatari kwa watoto na walimu kuangukiwa na majengo ya shule hiyo. 
Pangaselo
 alisema kwa sasa hali ya uchumi katika Kata hiyo sio nzuri kutokana na 
kuwa na changamoto ya ukosefu wa ajira kwa vijana hali ambayo imekuwa 
ikirudisha maendeleo nyuma.

 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
0 comments:
Post a Comment