Mkuu
wa Jeshi la polisi nchini (IGP), Simon Sirro amewataka makamanda wa
polisi mikoa kuhakikisha wanatumia vizuri mafuta ya magari wanayowekewa
ili kuepuka malalamiko ya wananchi kwa magari ya polisi kukosa mafuta.
Pia amesema hataki kusikia polisi hawajafika katika tukio kutokana na kisingizio cha kutokuwa na mafuta.
IGP
Sirro alisema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari jana
mkoani Morogoro na kuongeza kuwa ni kosa kwa mwananchi kudaiwa fedha za
mafuta ya gari la polisi.
IGP Sirro yupo katika ziara ya kuangalia hali ya uhalifu katika mikoa akitokea mkoani Dodoma.
Alisema
mafuta ya gari yapo katika bajeti ya Jeshi la Polisi kwa kila mkoa
hivyo kinachotakiwa ni makamanda wa mikoa kuhakikisha kuwa wanayatumia
vizuri.
“Ni jambo la kusikitisha mwananchi kutakiwa kuchangia mafuta ya gari la polisi,hili hatuliruhusu kabisa,” alisema Sirro
Hivi
karibuni, wakazi wa Malinyi walimlalamikia Mkuu wa Wilaya hiyo Jacob
Kassema kwa kuwachangisha Sh800,000 za mafuta ya gari lake. Hata hivyo,
Kassema alikanusha suala hilo.
Mbali
ya suala la mafuta, IGP Sirro aliwatoa hofu wananchi na kusema Serikali
inaendelea na uchunguzi wa kina kuhusu mauaji yanayoendelea mkoani
Pwani.
“Ni
kweli kuna tatizo la mauaji Pwani lakini askari wetu wapo kazini mchana
na usiku kutafuta suluhisho la tatizo,” alisema Sirro.
0 comments:
Post a Comment