1.Niko mbele yenu sio kufanya kampeni ya urais, niko mbele yenu kuomba ridhaa ya yenu kugombea nafasi ya urais muda ukifika.
2. Siko hapa kumlaumu mtu au ukimshambulia kwa sababu ukimlaumu mtu umAsikini bado uko palepale. Nikisema historia yangu yote muda hautatosha, kisomo nimesoma mpaka mwisho wa kusoma, kama ni taalumu nimefikia mwisho.
3.Nimepata bahati ya kusoma vyuo vikubwa sana duniani na sehemu kubwa nimepatia Ujerumani ndio maana wengine wanasema nafanya kazi kijerumani.
4.
Nimefanya utafiti kwa miaka 30,chama cha majiologia wamerekani
kilichoanza mwaka 1988, mimi niko ngazi ya juu pia kwa waingereza na
wachina niko ngazi ya juu kabisa.
5.Kwenye
uasisi mwaka 1976, CCM inaanza 77 sisi ndo waasisi, kadi hii hapa. Kama
nimeweza kutunza kadi ya CCM tangu 75 basi mimi ndio naweza kutunza
rasilimali zenu.
6.Toka tunapata uhuru tuna vikwazo, ujinga, maradhi na umasikini Mwl alitueleza. Nil lazima matatizo yatakuwepo kwenye jamii.
7.Rushwa
kubwa na ndogo, ukosefu wa ajira, siasa imekwenda kila mahala, taifa
linanyemelewa na uvuvu na utegemezi, dhulma, upungufu wa upatikanaji wa
takwimu sahihi, tumepungukiwa ushindani kama taifa, tumeshindwa
kujiamini.
8. Haya ndio nataka kuyashughulikia mimi. Upungufu wa mshikamano wa taifa letu. Kwetu asilimia 51 waislamu na 49 wakristo hivyo matatizo ya madhehebu hapa ndipo mahala pake. Afrika ina nchi 54, mimi nimeeenda 52 kasoro Mauritania na Chad. Ningekua sio muaminifu nisingepokelewa huko, ulaya nimezunguka.
8. Haya ndio nataka kuyashughulikia mimi. Upungufu wa mshikamano wa taifa letu. Kwetu asilimia 51 waislamu na 49 wakristo hivyo matatizo ya madhehebu hapa ndipo mahala pake. Afrika ina nchi 54, mimi nimeeenda 52 kasoro Mauritania na Chad. Ningekua sio muaminifu nisingepokelewa huko, ulaya nimezunguka.
9.Lazima
Tujue hali halisi ya uchumi wetu, chukueni kalamu na karatasi. Lazima
useme unatoka wapi unaenda wapi! India asilimia 74 wanajua kusoma na
kuandika. Nchi inayoongoza kwa watafiti ni Finland.(Anataja takwimu za
nchi ambazo tulikuwa tunafanana uchumi baada ya vita ya pili ya dunia
ikiwemo India, Brazil, China na Kenya.) Sipendi sana kujilinganisha na
Kenya kwa sababu sote ni maskini.
10.Dira
ya maendeleo inasema miaka kumi kutoka sasa Tanzania isiwe nchi
masikini, tusikae pembeni, tusogee juu kidogo. Hakuna mwenye uwezo huo
ni mimi tu ili tufikie pato la dola bilioni 200 kutoka dila bilioni 40.
Mwaka 2025 tutakuwa milioni 60, nataka tule miogo na viazi kwa hamu na
sio kwa shida.
11.Siwezi
kukupa ahadi ya mishahara wakati sijakuza uchumi, siwezi kukupa ahadi
ya kukujengea shule wakati sijakuza uchumi, tukuze kwanza uchumi.
12.Naombeni
ridhaa yenu nisimamishe deni la taifa lisiongezeke, mwenye dawa ya
umaskini ndani ya CCM, CHADEMA, NCCR ni profesa Muhongo tu. Elimu
kuiboresha lazima tuongeze bajeti, haiwezekani darasa limerundikana
ukafundisha. Anaeweza ni mimi tu sababu wengine utafiti wanausoma kwenye
magazeti tu.
13.Wana
CCM mnae mwanasayansi wa dunia, si mnipe tu! Tutatumia rasimali, madini
yetu tumeyachimba kwa asilimia 10 kitu, mimi ndio nimetengeneza ramani
ya madini ya Tanzania, Africa na duniani nikiwa vice president.
Nilizunguka hii nchi kuchora ramani ya madini kwa uzalendo, ningiweza
kuja na ramani na kuuzia serikali.
14.
Mimi mtu anidanganyi, unakuja tunajadiliana, hii sio dunia ya
kuandikiwa tu, inabidi na wewe ujiandikie. Niliweka mipango ya
kuwapunguzia bei ya umeme. Ilibidi nitoke kidogo mpate machungu
mnichague.
15. Nawaomba ifike mahala ifike mahala tuachane na matumizi ya kuni na mkaa, ni aibu sana. Tutajenga mabomba nchi nzima gesi itumike majumbani. Kila nyumba iwe na mabomba mawili, la maji na la gesi.
15. Nawaomba ifike mahala ifike mahala tuachane na matumizi ya kuni na mkaa, ni aibu sana. Tutajenga mabomba nchi nzima gesi itumike majumbani. Kila nyumba iwe na mabomba mawili, la maji na la gesi.
16.Wengine
mnaweza kuwadanganya, mimi hamuwezi kunidanganya, gesi yenu ipo kwenye
mikono ya uhakika kwa professa Muhongo tangu nimeanza kusoma wakati niko
chuo kikuu cha Dar es Salaam na nimefanya maisha yangu yote.
17.Mapato
ya gesi yasiende hazina, tutafungua mfuko maalumu na bunge litakua
linaizinisha asilimia ngapi iende kwenye bajeti. Mtanzania yoyote asiwe
na maamuzi ya kutumia hizo fedha bila idhini ya watanzania.
18.Mimi
sipendi wawekezaji wababaishaji na si kwamba sipendi wawekezaji wa
ndani, haya yote ya ujenzi wa uchumi lazima tuwe na umeme. Na umeme wa
bei nafuu ndio kazi niliyokuwa naianza. Umeme ulikuwa haukatiki mara kwa
mara, muda umefika tusijidharau, lazima tushinde.
19.Lazima
watanzania zaidi ya asilimia zaidi ya 75 wawe wanatumia umeme,
tutatumia vyanzo vyote vya umeme. Lazima mtembee kifua mbele professa
Muhongo amitimiza ahadi ya CCM, hata ilani mpya inayokuja mtekelezaji
atakaetekeleza kwa uhakika ni professa.
20.Ni
lazima tupambane na rushwa, na sio maneno kupambana nazo na nyie
wananchi muwe na uelewa na haki zetu. Mnaombwa rushwa kwa sababu hamjui
haki zenu. Naomba ridhaa yenu mniteue niwe mgombea wenu. Wakulima na
wafugani ni mwisho wa kuuana chini ya prof Muhongo, tatizo sio ardhi, ni
technologia.
21.Uwezo ninao, maarifa ninayo, jinsi ya kutafuta fedha ndani na nje, ambacho sina ni nyinyi kuniteua tu.
0 comments:
Post a Comment