KOCHA Rafa Benitez alijikuta anamwaga machozi wakati anatimiza ndoto yake ya maisha alipotambulishwa kuwa kocha mpya wa Real Madrid.
Mzaliwa huyo wa Madrid na kocha wa zamani wa Liverpool alitoa moja ya hotuba za awali iliyosisimua kuliko makocha wote waliofundisha klabu hiyo kwa miaka 15 iliyopita.
‘Ni hisia zinakuja upande wangu,"amesema. "Sijui kipi cha kusema. Nataka kuhakikisha tunashinda vitu na timu inacheza vizuri,"amesema.
Rafa Benitez was visibly emotional upon being unveiled as the new Real Madrid manager on Wednesday
Rafa Benitez alishindwa kuzuia hisia zake na kumwaga machozi wakati akitambulishwa kuwa Real Madrid
WASIFU WA RAFA BENITEZ
Kuzaliwa: Aprili 16, 1960
KLABU ALIZOCHEZEA
Real Madrid Castilla (1974-1981), Parla (Mechi 124 za Ligi, 1981-1985), Linares (Mechi za 34 ligi, 1985-1986).
TIMU ALIZOFUNDISHA
Real
Madrid B (1993–1995), Valladolid (1995–1996), Osasuna (1996),
Extremadura (1997–1999), Tenerife (2000–2001), Valencia (2001–2004),
Liverpool (2004–2010), Inter Milan (2010-2011), Chelsea (2012–2013),
Napoli (2013–2015), Real Madrid (2015–present)
MATAJI ALIYOSHINDA
VALENCIA
La Liga: 2001–02, 2003–04; UEFA Cup: 2003–04
LIVERPOOL
Kombe la FA: 2005–06; Ligi ya Mabingwa Ulaya: 2004–05; Super Cup: 2005
INTER MILAN
Super Cup ya Italia: 2010; Klabu Bingwa ya Dunia ya FIFA: 2010
CHELSEA
Europa League: 2012–13
NAPOLI
Coppa Italia: 2013–14; Super Cup ya Italia: 2014
Perez alisema: "Tunashawishika kuwasili kwa Benitez kutatufanya tuwe wa nguvu. Tunamleta kocha ambaye wakati ametaka kuwa kocha wa klabu hii. Mtu fulani mmoja ambaye anafahamika kwa juhudi zake na utaalamu,".
Perez alisoma orodha ya mataji ambayo Benitez amewahi kushinda katika timu alizofundisha likiwemo la Ligi ya Mabingwa alilolitwaa akiwa na Liverpool na mawili ya La Liga aliyochukua alipokuwa Valencia.
Akasema: "Anaifahamu hii klabu. Ni mmoja wetu. Alifika hapa akiwa na umri wa miaka 13 na nafikiri ni maalum sana kwake kupewa timu kama kocha leo. Mpendwa Rafa, karibu nyumbani.’
Benitez alitambulishwa kama kocha mpya wa Madrid katika Mkutano na Waandishi wa Habari leo baada ya ziara ya kutembezwa katika Uwanja wa mazoezi wa klabu, Valdebebas.
Alipata fursa ya kusalimiana na kocha gwiji wa klabu, Iker Casillas, ambaye inasemekana mikoba yake kama kocha namba moja wa Hispania na Real Madird itarithiwa na David De Gea msimu ujao.
"Leo si siku ya kuzungumzia masuala binafsi. Nataka kufurahia vipaji vikubwa navyokwenda kukutana navyo katika timu,".
Na badaye alipoulizwa; "Unafikiri nini kuhusu Casillas kama kipa?’ akarudia alichosema; "NImesema kabla, sifikiri nitazungumzia kuhusu mchezaji mmoja mmoja na hata kujibu swali hili,".
0 comments:
Post a Comment