Pages

Ads 468x60px

Saturday, June 6, 2015

Bodaboda Kuanza Kukatiwa bima Kubwa..



KAMPUNI ya Bima ya Zurich Brokers (EA) Ltd imeanza mchakato wa kuwaondoa waendesha bodaboda jijini Mwanza katika bima ndogo ya Sh 10,000  hadi Sh 125,000.

Akizungumza Mwanza juzi, Meneja wa Zurich Insurance Broker (EA) Ltd, Kanda ya Ziwa, Curtis Mukami, alisema wameamua kumsafirisha kiongozi mmoja wa bodaboda hadi Dar es Salaam ili kufanya mazungumzo ya kuwasaidia kukata bima ya Sh 125,000.

Alisema kampuni yao imepokea taarifa ya bodaboda hao jinsi wamiliki wa pikipiki wanavyokata bima ndogo ambayo haiwasadii pale wanapopata ajali au tatizo lolote.

“Tunapozungumza hapa, Mwenyekiti wa  Shirikisho la Machinga Manispaa ya Ilemela, Dennis Nyamlekela yupo Dar es Salaam, viongozi wetu wa kitaifa watakaa na wauzaji wa pikipiki, bajaji, magari ili kuweka mkakati wa pamoja na kuwaokoa madereva.

“Tunataka kila mwendesha pikipiki, mmiliki pamoja na mtu atakayekuwa ameguswa kwa namna yoyote na ajali au tatizo la chombo hicho alipwe, lakini kama dereva hatakuwa na leseni na kwa bahati mbaya akapata ajali, hapo hatalipwa, hivyo hivyo na mmiliki,” alisema Mukami.

Naye Ofisa Huduma kwa Wateja wa Zurich, Hyasinta Tarimo, alisema Watanzania wengi wamekuwa wakikata bima ya moto kwa ajili nyumba zao, lakini wanashindwa kutambua kuna bima ya wizi na majanga, yakiwamo mafuriko.

Alisema asilimia 98 ya Watanzania wanaomiliki nyumba zao hawana bima ya  mali zao zilizomo ndani ya nyumba na majanga.

Alisema baada ya kampuni hiyo kuzinduliwa Mwanza, kumekuwapo na mwitikio mkubwa wa wamiliki wa pikipiki, magari, nyumba na afya na kwa mwezi mmoja wamefanikiwa kupata wanachama zaidi ya 400.

“Kikubwa tunawaomba wamiliki wa shule binafsi, vyuo, madhehebu, hospitali kukata bima ili kuweka mali zao salama, baada ya kuzinduliwa kampuni yetu, tumebaini watu hawana uelewa wa bima isipokuwa wale watumishi wa umma na mashirika,” alisema Tarimo.

0 comments:

Post a Comment

SHARE