Taarifa kutoka kwa waziri wa mambo ya ndani Joseph Nkaissery inaeleza kwamba, watu 14 wamekamatwa kuhusiana na shehena ya pembe za ndovu zilizosafirishwa hadi Thailand, na fedha kulipwa kundi linalopigania kujitenga kwa pwani la Mombasa Republican Council, MRC.
Wakuu wa kundi hilo lililopigwa marufuku, wanasisitiza kwamba lengo lao ni kutetea haki na uhuru wa waislamu wa Kenya. Imekanusha mara kwa mara kuhusika na mlolongo wa mashambulizi katika eneo la pwani la taifa hilo.
0 comments:
Post a Comment