Pages

Ads 468x60px

Sunday, June 7, 2015

Tanzania Yadaiwa Kuwa Kitovu Cha Ujangili wa Tembo Afrika


Tanzania imedaiwa kuwa kama kitovu cha tatizo la ujangili wa Tembo, baada ya sensa ya serikali ya Tanzania, kubaini imepoteza asilimia 60 ya Tembo katika miaka mitano iliyopita.
Ripoti ya serikali ya Tanzania, iliyotolewa Jumatatu, inakadiria Tembo 65,721 wamekufa nchini humo katika muda wa miaka mitano iliyopita.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, Tembo wa Tanzania wamepungua kutoka 109,051 mwaka 2009 na kufikia 43,330 ilipofika mwaka 2014.
Mkuu wa kundi la uhifadhi TRAFFIC, Steven Broad, amesema kiwango hicho cha ujangili kinashangaza kutotambuliwa na kushughulikiwa kabla ya sasa.
Amesema idadi hiyo ni maafa na kuishutumu Tanzania, kwa hali hiyo ya Ndovu.
Kwa mujibu TRAFFIC, tani 45 za pembe za ndovu zilifika katika masoko gharamu kutoka Tanzania, toka mwaka 2009, na kuifanya kuwa sehemu ya kwanza kwa ujangiri wa pembe za ndovu barani Afrika.
Serikali ya Tanzania imesema imeongeza walinzi zaidi 1,000 wa wanyama pori, lakini Bwana Broad, amesema hatua hiyo inaweza kuwa imechelewa katika kulinda idadi ya Tembo.

0 comments:

Post a Comment

SHARE