Pages

Ads 468x60px

Thursday, June 4, 2015

R.I.P>> Pinda aongoza wabunge kumuaga mbunge wa Ukonga Aliyefariki Dunia Juzi


Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akitoa heshima za mwisho kwa aliyekuwa mbunge wa Ukonga Eugen Mwaiposa kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Juni 3, 2015.
 
Mwili wa marehemu Mhe. Eugen Mwaiposa aliyekuwa mbunge wa Ukonga ukiwasili kwenye viwanja vya bunge jana  mjini Dodoma kwa ajili ya kuagwa.
 
Katibu Mkuu Kiongozi Mhe. Balozi Ombeni Sefue, Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai, Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda, Mbunge wa Singida Mashariki Mhe. Tundu Lissu, Mbunge wa Monduli Mhe. Edward Lowassa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Bibi Chiku Galawa wakiwa kwenye shughuli ya kuaga mwili wa marehemu Mhe. Eugen Mwaiposa.
 
Wabunge Mhe. Anna Abdalla (kushoto) na Mhe. Ester Bulaya wakiaga mwili wa marehemu Mhe. Eugen Mwaiposa aliyekuwa mbunge wa Ukonga kwenye viwanja vya bunge jana  mjini Dodoma.
  ***
Waziri mkuu Mizengo Pinda pamoja na wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wameshiriki kuaga mwili wa aliyekuwa mbunge wa Jimbo la Ukonga Eugen Mwaiposa aliyefariki dunia juzi.
 
Shughuli ya kuaga mwili wa mbunge huyo ilifanyika jana mchana nyumbani kwa mbunge huyo maeneo ya Chadulu mjini Dodoma, na kuhudhuriwa pia na viongozi mbalimbali wa madhehebu ya dini na serikali akiwemo mkuu wa mkoa wa Dodoma, Kepteni mstaafu Chiku Galawa.
 
Katika salamu zake Naibu Spika wa bunge Mh. Job Ndugai  kwa niaba ya Bunge, aliuelezea msiba kuwa ni pigo kwa bunge na taifa kiujumla, kwa kuwa mambo mengi mazuri aliyokuwa nayo marehemu bado yalikuwa yanahitajika.
 
Kwa upande wao baadhi ya wabunge waliohudhuria shughuli hiyo kwa uwakilishi wa makundi yao walisema watamkumbuka marehemu kwa mengi ikiwa ni pamoja na uwezo wake wa kusimamia hoja mbalimbali za maendeleo katika jimbo lake.
 
Baada ya shughuli ya kuaga, mwili wa marehemu Mwaiposa ulisafirishwa kutoka Dodoma kwa njia ya Ndege na uliwasili alasiri nyumbani kipunguni Dar es salaam.
 
Mwili wa Mwaposa  utazikwa jijini  Dares salaam  katika eneo la Kipunguni  siku ya Jumamosi.

0 comments:

Post a Comment

SHARE