Pages

Ads 468x60px

Wednesday, June 10, 2015

Sitta awaonya wanasiasa chokochoko za muungano



Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi, Samuel Sitta amesema kuna wanasiasa wanafanya chokochoko za Muungano huku akisema ikiwa atafanikiwa atateuliwa na chama chake kuwania urais atawashughulikia.

Akizungumza na waandishi wa habari katika Kijiji cha Wawi alipozulu kaburi la Makamu wa Rais wa Tanzania, marehemu Dk. Omar Ali Juma, Waziri Sitta alisema kwamba kumejitokeza watu wanaouchimba Muungano akiwataka kuwa hawana nia njema.

“Nikifanikiwa kuteuliwa na chama changu kuwa mgombea na baadae kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania…nitaulinda na sitawavumilia wale wote wanaochezea Muungano wetu,” alisema Waziri Sitta.

0 comments:

Post a Comment

SHARE