Pages

Ads 468x60px

Wednesday, June 10, 2015

Mbunge aitaka Serikali ianzishe idara ya vipodozi



MBUNGE wa Mji Mkongwe, Ibrahim Sanya (Chadema), ameitaka Serikali kuanzisha elimu ya madhara ya vipodozi visivyo na viwango kwa shule za msingi.
 
Akiuliza swali bungeni jana, Sanya alisema kuanzishwa kwa elimu hiyo kunatokana na Serikali kushindwa kudhibiti uingizwaji wa vipodozi hivyo  nchini hali inayosababisha kuogezeka kwa matumizi.
 
“Kwa nini Serikali isishirikiane na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kuingiza elimu ya madhara ya vipodozi katika somo la sayansi ili wanafunzi wa shule za msingi wajue madhara yake ikiwemo kuonyeshwa picha za watu walioathirika?” alihoji.
 
Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Stephen Kebwe alisema progamu ya kufundisha madhara ya vipodozi kwa shule za msingi imeshaanza tangu mwaka 2009.
 
Awali akijibu swali la msingi la Sanya, Dk. Kebwe alisema Wizara yake kupitia Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) imeweka utaratibu wa kudhibiti uingizaji na utoaji nje ya nchi wa vipodozi pamoja na bidhaa nyingine inazozidhibiti.
 
“Hadi sasa jumla ya vipodozi 2,527 ndivyo vimeruhusiwa kuingizwa nchini.
 
“Vilevile katika mwaka wa fedha 2014/15 mabasi ya abiria matatu yalikamatwa mkoani Mbeya na Dar eas Salaam yakiwa yamebeba vipodozi ambavyo havijasajiliwa kutoka nchi jirani na wahusika kuchukuliwa hatua za kisheria.
 
“Katika mwaka 2014/15, jumla ya tani 16.61 za vipodozi vilivyopigwa marufuku vyenye thamani ya Sh. milioni44.2 zimeteketezwa na TFDA,” alisema Dk. Kebwe.
 
Alisema elimu imekuwa ikitolewa njuu ya matumizi sahihi ya vipodozi na kwamba mwaka 2014/15 shule 16 zilitembelewa na elimu kutolewa juu ya matumizi ya vipodozi.
 
Katika swali lake Sanya alitaka kujua lini Serikali itakuwa makini kuzuia vipodozi ambavyo havina viwango kuingia nchini.

0 comments:

Post a Comment

SHARE