Mbunge aitaka Serikali ianzishe idara ya vipodozi
Mpekuzi blog
MBUNGE
wa Mji Mkongwe, Ibrahim Sanya (Chadema), ameitaka Serikali kuanzisha
elimu ya madhara ya vipodozi visivyo na viwango kwa shule za msingi.
Akiuliza
swali bungeni jana, Sanya alisema kuanzishwa kwa elimu hiyo kunatokana
na Serikali kushindwa kudhibiti uingizwaji wa vipodozi hivyo nchini
hali inayosababisha kuogezeka kwa matumizi.
“Kwa
nini Serikali isishirikiane na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi
kuingiza elimu ya madhara ya vipodozi katika somo la sayansi ili
wanafunzi wa shule za msingi wajue madhara yake ikiwemo kuonyeshwa picha
za watu walioathirika?” alihoji.
Akijibu
swali hilo, Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Stephen Kebwe
alisema progamu ya kufundisha madhara ya vipodozi kwa shule za msingi
imeshaanza tangu mwaka 2009.
Awali
akijibu swali la msingi la Sanya, Dk. Kebwe alisema Wizara yake kupitia
Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) imeweka utaratibu wa kudhibiti
uingizaji na utoaji nje ya nchi wa vipodozi pamoja na bidhaa nyingine
inazozidhibiti.
“Hadi sasa jumla ya vipodozi 2,527 ndivyo vimeruhusiwa kuingizwa nchini.
“Vilevile
katika mwaka wa fedha 2014/15 mabasi ya abiria matatu yalikamatwa
mkoani Mbeya na Dar eas Salaam yakiwa yamebeba vipodozi ambavyo
havijasajiliwa kutoka nchi jirani na wahusika kuchukuliwa hatua za
kisheria.
“Katika
mwaka 2014/15, jumla ya tani 16.61 za vipodozi vilivyopigwa marufuku
vyenye thamani ya Sh. milioni44.2 zimeteketezwa na TFDA,” alisema Dk. Kebwe.
Alisema
elimu imekuwa ikitolewa njuu ya matumizi sahihi ya vipodozi na kwamba
mwaka 2014/15 shule 16 zilitembelewa na elimu kutolewa juu ya matumizi
ya vipodozi.
Katika swali lake Sanya alitaka kujua lini Serikali itakuwa makini kuzuia vipodozi ambavyo havina viwango kuingia nchini.
0 comments:
Post a Comment