JUMLA ya viongozi 73 wameshafikishwa mbele ya Baraza la Maadili katika kipindi cha mwaka 2010/11 hadi 2014/15.
Takwimu
hizo zilitolewa bungeni jana na Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais, Utawala
Bora, Kapteni George Mkuchika wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti
Maalumu, Fakharia Shomar Khamis (CCM),
Katika
swali lake Mbunge huyo alitaka kujua idadi ya viongozi ambao ahadi sasa
wameshafikishwa Sekretarieti ya Viongozi wa Umma kutokana na ukiukwaji
wa maadili.
Mkuchika
alisema viongozi hao walifikishwa kwa sababu mbalimbali zikiwemo
kushindwa kutoa tamko la rasilimali na madeni, matumizi mabaya ya
madaraka, kutoa tamko la uongo, kutotamka maslahi ya mkataba na Serikali
na kutotamka zawadi.
“Kati
ya malalamiko 73 yaliyofikishwa mbele ya Baraza, viongozi 18
hawakupatikana na hatia, 29 walipatikana na hatia na kupewa adhabu
mbalimbali,” alisema.
Alisema watumishi 14 walipewa onyo, 10 walipewa onyo kali, wanne walipewa onyo na tahadhari na kiongozi mmoja alitozwa faini.
“Malalamiko 26 yaliyobakia yako kwenye hatua mbaalimbali ikiwemo malalamiko 17 ambayo yameahirishwa kusikilizwa na Baraza.
“Malalamiko
matatu yanasubiri uamuzi wa Mahakama Kuu kufuatiwa walalamikiwa kuomba
kupinga uamuzi mdogo wa Baraza wa kuendelea kuwachunguza,” alisema.
Mkuchika alisema Baraza limakubali lalamiko moja liendelee katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
“Malalamiko
matano yamekamilika na taarifa yake imewasilishwa kwenye mamlaka husika
kwa utekelezaji wa mapendekezo ya Baraza la Maadili,” alisema.
0 comments:
Post a Comment