Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Muliro Jumanne Muliro akiwa eneo la tukio-Picha na Marco Maduhu
***
Mwendesha bodaboda aliyejukana kwa jina
la Joel Gabriel Mamla amefariki dunia baada ya kupasuka kichwa
akikimbizana na askari wa usalama barabarani mjini Shinyanga.
Kwa Mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo
wanasema mwendesha bodaboda huyo amepoteza maisha kwa kuanguka kwenye
pikipiki aliyokuwa amembeba askari polisi aliyekuwa amevaa kiraia.
Kufuatia kifo hicho wananchi waliamua
kumshushia kichapo askari polisi huyo na jeshi la polisi kulazimika
kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya wananchi waliokuwa wanamtuhumu
kusababisha kifo hicho.
"Tulishuhudia mwendesha bodaboda
akivutana na askari polisi baada ya kumkaba shingoni bila kuelewa sababu
na baadae ajali ikatokea"
"Wamekuja wanavutana kwenye
pikipiki,walikuwa wanakabana juu ya pikipiki,walipofika eneo ambako
yanatokea mabasi,askari akawa anaburuza miguu chini,mara akamkaba
mwendesha bodaboda ili pikipiki isimame,askari akamkaba roba
dereva,ikabidi aachie usukani,alivyotaka kurudi akakuta pikipiki
imeshahama barabarani ndiyo akakutana na alama ya barabarani
akaibamiza,akaangukia jiwe ndivyo kifo chake kilivyotokea,sisi tulijua
huyo askari pengine ni raia maana hakuvaa kiraia",mashuhuda wa tukio hilo wanasimulia hali ilivyokuwa.
Mganga Mfawidhi wa hospitali ya rufaa ya
mkoa wa Shinyanga,Dkt. Herbert Masigati amethibitisha kutokea kwa kifo
cha mwendesha bodaboda huyo na kuongeza kuwa alipasuka kichwa baada ya
ajali kutokea.
Taarifa ya jeshi la polisi mkoa wa
Shinyanga kwa vyombo vya habari kuhusiana na ajali ya pikipiki kuanguka
na kusababisha majeruhi kwa askari na mwendesha pukipiki (bodaboda)
Tarehe 6/6/17 majira ya saa 1245 eneo la
Soko kuu Manispaa ya Shinyanga, askari mmoja mwenye cheo cha CPL wa
kikosi cha usalama barabarani akiwa na askari wenzake wawili wakiwa
katika utekelezaji wa majukumu yao ya kisheria ya ukamataji wa kawaida
wa waendesha pikipiki zisizotii sheria za barabarani,waliikamata
pikipiki na MC 700 AWH SANLG iliyokuwa ikiendeshwa na Joel Gabriel
Mamla, 26yrs kwa kosa la kutovaa helmet.
Mtuhumiwa huyo aliwakuta askari hao eneo
la Soko Kuu na baada ya kushusha abiria ndipo alipoambiwa kosa lake na
kuamriwa kwenda kituo cha polisi kwa hatua zaidi za kisheria.
Dereva huyo wa bodaboda alidai yeye
ndiye atakayeendesha pikipiki yake na hivyo akampakia kwa nyuma askari
polisi aliyekuwa amevaa kiraia aliyepewa jukumu na kiongozi wake
ampeleke mtuhumiwa kituoni.
Badala yake dereva huyo wa bodaboda
alibadilisha uelekeo wa barabara baada ya kutoka pale sokoni na kuanza
kuendesha kwa speed kubwa kuelekea barabara ya Tabora- Tinde huku
akimweleza askari yule kuwa watakufa wote.
Alipofika eneo la Buhangija aliielekeza
pikipiki kwenye nguzo ya alama ya usalama wa barabarani na akafanikiwa
kuitumbukiza kwenye shimo kwa maksudi ambapo wote walianguka na hivyo
kupata majeraha na wakakimbizwa hospitali ya mkoa kwa matibabu.
Uchunguzi wa kina kuhusiana na tukio hili unafanywa.
Hali zao ni mbaya.
Imetolewa na Muliro J Muliro RPC - Shinyanga.
0 comments:
Post a Comment