Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe akionesha mkoba wenye fomu za kugombea urais katika ukumbi wa mikutano wa NEC mjini Dodoma.
********** 
  
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la 
Nachingwea, Mathias Chikawe jana amechukua fomu ya kuomba ridhaa ya 
 kugombea Urais kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi katika uchaguzi mkuu 
utakaofanyika mwezi oktoba 2015.
Akizungumza mara baada ya kuchukua fomu Chikawe alisema akiteuliwa na
 chama chake kugombea nafasi hiyo ataendeleza mapambano zaidi dhidi ya 
maadui watatu ambao ni ujinga, maradhi na umaskini pamoja na adui 
mwingine rushwa ambaye  ni adui wa maendeleo.
Waziri Chikawe aliongozana na mke wake pamoja na wapambe 
mbalimbali ambao walikuwa wakimshangilia wakati wa kujibu maswali ya Waandishi
 wa Habari  katika wa ukumbi wa  Mkutano mkuu wa NEC.


 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
0 comments:
Post a Comment