Pages

Ads 468x60px

Tuesday, June 9, 2015

BASATA wambana Amanda Poshi, wazuia shoo yake>>>



Msanii wa filamu nchini Tanzania, Tamrina Poshi ‘Amanda’ amejikuta katika wakati mgumu baada ya BASATA, kumzuia kufanya shoo aliyopanga kufanya wiki iliyopita kutokana na kualika vikundi vya burudani ambavyo vipo kinyume na maadili.
 
Amanda, amesema kuwa shoo hiyo ilikuwa ifanyike katika ukumbi wa Mzalendo, Kijotonyama jijini Dar es Salaam, lakini ilishindikana kutokana na kupokea barua kutoka BASATA ya kusitisha shoo hiyo.
 
Amedai kwa mujibu wa BASATA vikundi vya baikoko na khanga moko walivipiga marufuku kufanya shoo kutokana na kuvaa mavazi ya nusu utupu hivyo kushindikana kufanyika kwa shoo hiyo.

0 comments:

Post a Comment

SHARE