Mtangazji wa redio nchini Tanzania, Dina Marious, baada ya kuwa kimya
bila kusikika katika vipindi vya redio muda mrefu amejitokeza na
kufunguka siri ambazo watu wengi walikuwa hawajui baada ya kuulizwa mara
kwa mara sababu za kutosikika redioni.
Kupitia mtandao wa kijamii amesema “Katika haya maisha hamna kitu
kibaya kama kumuonea na kumnyanyasa mtu ambaye hana hatia.Kwa kutumia
cheo,madaraka,nguvu na nafasi uliyonayo ukiamini huyo mtu hana uwezo wa
kukufanya lolote”.
“Tunaishi katika dunia ambayo binadamu wamekosa utu na imani.Binadamu
wamekuwa wanyama na makatili kuliko wanyama wenyewe.Unaweza ukakutana
na simba na chui porini mkakaa mkatia story lakini sio binadamu”.
“Unafanyiwa unyama eti kisa wanataka revenge kwa mtu wako wa
karibu.Ambae revenge hiyo wala haimuathiri lolote zaidi ni kukutesa wewe
kisaikolojia siku hadi siku. Mbaya zaidi sikustahili miaka yote
nimejituma,nimejitoa,sijawahi kumvunjia heshima alokuwa juu yangu kwa
ngazi zoote”.
“Ndugu zangu nimeishi kwa muda mrefu katika huzuni,msongo wa
mawazo.Na hapa niliponimedevelop na vidonda vya tumbo.Nimekuwa na kitu
kifuani kimenikaaa kila siku nahisi nisiposema nitakufa.Ningekuwa
nimetendewa haki isingeniuma wala kunisumbua ni kwa sababu nimeonewa
sanaa tena katika kipindi kibaya sana”.
“All this time nimekuwa mnyenyekevu na najichekesha nakujitabasamisha
machoni pa watesi wangu.Na wao wakiendelea kunikanyagia chini bila
huruma huku wakinichekea”.
“Leo nimeamka nina huzuni sana sana na ninahuzunika hasa ninapokutana
na msg za kuniuliza niko wapi?mbona sisikiki?? Mimi bado ni muajiriwa
na ninalipwa mshahara ila nimewekwa benchi tu”.
“Kuna kitu naomba nikiweke clear kumekuwa na maneno mengiiiiii
yanazunguka kuwa nina ugomvi na Zamaradi.Mimi sina ugomvi na Zamaradi
sijui ndio amechangia mimi kutolewa kwenye leo tena.Thats not true wala
nguvu hiyo hana.Sijajua why watu husema hivyo ila sina ugomvi nae.Hata
yeye anajua hatuna ugomvi wowote.Nilipotoka pale niliamua kubadili mfumo
wangu wa maisha hivyo hatuna ukaribu kama zamani.Ila haimaainishi tuna
ugomvi”.
“Na malizia kwa kusema sipo radio wala sipo tv kwa sasa.Maswali
mnaniuliza kila siku na nina wajibu kila mara na leo nimewajibu
tena. ila nitakuwa kwa radio na tv hapo baadae acha niuze mafuta ya
nazi.Maelezo ya mwanzo yamejitosheleza sanaa na sitaenda mbalii sanaa
labda nikiandike kitabu ndio yatatimia”.
“Nimeandika haya kwa ufupi mjue hata sisi pamoja na majina tuliyonayo
changamoto zipo na tunakabiliana nazo.Na ipo siku tutashinda maana
mtetezi wetu yu hai”.
0 comments:
Post a Comment