Katika hali isiyo ya kawaida Askofu Mkuu wa Kanisa la Full Gospel
Bible Fellowship, Zachary Kakobe amefunguka na Injili nzito kwa kuwataja
baadhi ya wagombea urais kwamba waingie katika wokovu kamili badala ya
kuwa na wokovu aliodai ni wa kuigiza.
Katika moja ya mahubiri yake kanisani kwake Mwenge, Sam Nujoma Road,
Askofu Kakobe aliwataja wagombea urais Mwingulu Nchemba na Lazaro
Nyalandu pamoja na mmoja wa mawaziri maarufu, Dk. Harisson Mwakyembe
kwamba wanapaswa kuokoka ili mambo yao yawanyokee.
“Leo sikwepeshi maneno. Kila mtu anajifanya ameokoka lakini huo ni
wokovu ule. Nyalandu (Lazaro), ameokoka kweli? Mwigulu (Nchemba),
ameokoka kweli, Mwakyembe (Dk. Harisson) ameokoka? Angalia sasa kwa
viwango hivi ndiyo utajua umeokoka au namna gani.
“Mimi hapa sitafuti mtu, waziri ukija hapa, rais ukija hapa
utanisaidia nini, rais huwezi kunipa hela mimi….mimi ndiyo naweza kumpa
hela…sihitaji hela ya mwanasiasa, ninachohitaji watu waingie katika
wokovu wa kweli,” alisema Askofu Kakobe.
Nyalandu aliwahi kuonekana katika kanisa linaloongozwa na Nabii
Josephat Mwingira Kibaha ambako aliwaomba waumini kumuunga mkono katika
harakati zake za urais na Dk. Mwakyembe aliwahi kuonekana katika Kanisa
la Askofu Josephat Ngwajima.
Hata hivyo, Mwigulu naye kwa mujibu wa Askofu Kakobe, amekuwa
akijitangaza kwamba ameokoka, wokovu ambao kiongozi huyo haridhiki
nao.Hakuna kiongozi yeyote kati yao aliyepatikana juzi kuzungumzia wito
huo wa Askofu Kakobe.
0 comments:
Post a Comment