Pages

Ads 468x60px

Wednesday, June 10, 2015

Mwandosya Awataka Wagombea Urais CCM Waache Kuwajadili na Kuwasema Vibaya Wagombea Wenzao!



WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais (Kazi Maalumu), Profesa Mark Mwandosya, ameonya wanaojadili wengine badala ya hoja katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu kuwa hawawezi kuisaidia nchi kwa mtindo huo.
 
Profesa Mwandosya alisema hayo mjini hapa jana, alipokuwa akitafuta wadhamini ambao CCM imewataka kwa mtu anayetangaza nia ya kugombea urais na kuchukua fomu.
 
Kwa mujibu wa matakwa ya chama hicho, anayetangaza nia na kuchukua fomu za kugombea nafasi hiyo anapaswa kutafuta wadhamini 450 kutoka mikoa 15 ya Tanzania Bara na Zanzibar.
 
Alisema ukiona mtu anaacha hoja ya msingi na kuanza kumjadili mtu, ujue kuwa hana busara na hajakomaa kisiasa.
 
Kwa maelezo ya Profesa Mwandosya, wanaotangaza nia wanapaswa kuwaeleza wananchi jinsi watakavyotatua kero zao na kuwaletea maendeleo, hivyo suala la msingi la kujadiliwa linafaa kuwa hoja za mtangaza nia, kuona endapo zina mantiki au la.

0 comments:

Post a Comment

SHARE