IMEELEZWA kuwa katika wilaya ya Bunda, mkoani Mara, kuna watoto wanaofikia 92 wanaoishi na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi.
Taarifa hiyo ilitolewa jana na Ofisa Maendeleo ya Jamii katika Wilaya
ya Bunda, Caroline Wanzagi.
Wanzagi alisema kuwa watoto hao wanaendelea kupata huduma ya matibabu
na misaada mbalimbali kutoka katika mashirika, taasisi na serikalini.
Alisema kuwa watoto hao wamepata maambukizi hayo kutokana na sababu
mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kuyapata kutoka kwa mama zao wenye
maambukizi, unyanyasaji wa kijinsia ukiwamo ubakaji na ajira hatarishi.
Alisema kuwa ili kupunguza idadi ya maambukizi ya VVU kwa watoto
kutoka kwa mama mwenye maambukizi au maambukizi yanayoweza kutokea kwa
watoto kutokana na unyanyasaji, ubakaji na ajira hatarishi, ni muhimu
kuelimisha jamii juu ya changamoto hiyo, ili kuzuia maambukizi hayo.
Aliongeza kuwa pia ili kukabiliana na changamoto hiyo ni muhimu
wazazi wote yaani mama mwenye ujauzito na baba wahudhurie huduma za
klini, ili kumsaidia mtoto aliyeko tumboni kuzaliwa bila maambukizi ya
VVU.
Alisema kuwa hali hiyo itasaidia kupunguza idadi ya watoto
wanaozaliwa na maambukizi ya VVU, kwa kuwa wazazi wote watawajibika
katika afya zao na afya ya mtoto, ikiwa ni pamoja na mtoto kupata huduma
ya option B kwa mama ndani ya masaa 72 kabla ya uchungu.
“Hii itasaidia kupunguza idadi ya watoto wanaozaliwa na maambukizi ya
VVU kwa kuwa wazazi wote watawajibika katika afya zao na afya ya mtoto,
ikiwa pia na mama kupata huduma ya ndani ya masaa 72 kabla ya uchungu,”
alisema.
Alisema kuwa baba na mama kuhudhuria klini itasaidia baba kufanya
maandalizi ya kumwezesha mama kujifungulia kwenye kituo cha afya au
hospitalini na hivyo kumkinga mtoto asipate maambukizi ya VVU, ikiwa ni
pamoja na kuondoa usiri wa matumizi ya ARV.
0 comments:
Post a Comment