Showing posts with label Entertainments. Show all posts
Showing posts with label Entertainments. Show all posts
Monday, August 15, 2016
Wednesday, August 10, 2016
A New Travelers Social Network is Here..Check It Out
makers and those who simply enjoy exploring the world.
Tuesday, July 12, 2016
Thursday, July 9, 2015
Nassari Afunguka.......Asema Ajali ya Helikopta Aliyopata ni ya Kishirikina, Ndesamburo Asema Atanunua Nyingine>>
Wakati Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari akisema anashindwa kuamini kilichotokea na kunusurika katika ajali ya helikopta juzi, mmiliki wa chopa hiyo, Philemon Ndesamburo amesema atanunua nyingine haraka kabla ya kuanza kampeni za Uchaguzi Mkuu.
Kauli hizo zilitolewa jana ikiwa ni siku moja
baada ya helikopta hiyo inayomilikiwa na Ndesamburo kupitia kampuni yake
ya Keys Aviation kupata ajali wakati ikitumiwa na Nassari na baadhi ya
viongozi wa Chadema.
Wakati ikipata ajali, ilikuwa imekodishwa na Kampuni ya General Aviation Services (T) Ltd inayomilikiwa na Kapteni William Slaa.
Katibu wa Ndesamburo, Basil Lema alisema ilipata
ajali baada ya kupigwa na kimbunga wakati anga likiwa limefunikiwa na
wingu zito.
“Mheshimiwa Ndesamburo amemshukuru Mungu kwa
kuwanusuru watu waliokuwa kwenye ndege hiyo ambao ni pamoja na Mbunge
Joshua Nassari.
“Ameweka wazi kwamba atalazimika kununua nyingine
mapema kwa ajili ya kuongeza nguvu kwenye kampeni za Uchaguzi Mkuu mwaka
huu,” alisema Lema akimnukuu Ndesamburo.
Lema alisema rubani aliyekuwa akiendesha helikopta
hiyo alifanikiwa kuielekeza juu ya miti alioutumia kupunguza kasi ya
kushuka chini na kusaidia abiria kutoka salama.
“Imeharibika lakini abiria wote ni wazima.
Walikuwamo wanne,” alisema na kuongeza kuwa helikopta hiyo ndiyo
iliyotumiwa na Chadema katika Uchaguzi Mkuu wa 2010 na Uchaguzi wa
Serikali za Mitaa mwaka jana na chama hicho kilitegemea kuitumia katika
Uchaguzi Mkuu ujao.
Pia, imewahi kutumiwa na makada mbalimbali wa CCM
akiwamo Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Mwigulu Nchemba na kada maarufu wa
Moshi mjini, Buni Ramole.
Kauli ya Nassari
Akizungumza na waandishi wa habari katika wodi
alikolazwa kwenye Hospitali ya Seliani – Arusha, Nassari alisema
waliporuka kutoka Leguruki, hakukuwa na dalili zozote za kuchafuka kwa
hali ya hewa, lakini dakika chache baada ya kuruka angani wingu zito
lililoambatana na upepo mkali liliwafunika ghafla.
“Wingu lile na upepo ule sijawahi kuona katika
maisha yangu yote zaidi ya kusoma kwenye vitabu vya simulizi vya mambo
ya ushirikina. Namshukuru Mungu wote tuko salama kwani hatukuwa na
matumaini ya kupona ajali ile,” alisema Nassari.
Mbunge huyo aliyekuwa katika ziara ya kuhamasisha wananchi
kujiandikisha kwenye Daftari la Wapigakura, alimwagia sifa rubani Slaa
kwa uwezo na ustadi aliouonyesha hadi wakanusurika.
“Kama siyo ustadi wake, naamini watu wangeokota
vipande vya nyama tu kwenye eneo la ajali, ila Mungu ni mkuu leo tuko
hai wote licha ya madhara madogo,” alisema.
Nassari alisema muda mfupi kabla ya kuruka saa
kumi na moja jioni, wakati akihutubia mkutano huko Leguruki, alipokea
simu kutoka kwa mchungaji mmoja akimtaarifu kupata maono kuwa
anakabiliwa na hatari ya kukutwa na jambo kubwa na baya akimtaka adumu
katika sala.
“Dakika 15 baadaye nikaruka na kupata ajali.
Naamini kilichotuokoa ni nguvu ya sala niliyosali baada ya kupokea
ujumbe wa mchungaji na maombi ya wachungaji wangu wanaoniombea kila
siku,” alidai Nassari.
Rubani Slaa alisema alishangaa lilipotokea wingu
na upepo uliosababisha ndege kuanguka ikiwa njiani kuelekea Ndoombo na
Ngureserosambu.
“Kabla ya kurusha ndege nilijiridhisha na hali ya
hewa. Hakukuwa na kiashiria chochote cha hali ya hatari kama maeneo
mengine ambako tulishindwa kutua kutokana na mvua zilizokuwa zikinyesha."
Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali ya Seliani, Dk Paul
Kisanga alisema hali za majeruhi si mbaya, isipokuwa Eva Kayaha
aliyevunjika mbavu mbili.
Sunday, July 5, 2015
Nyota ya Diamond Platnumz Inazidi Kung'ara.......Katajwa Kuwania Tuzo za Uganda (Uganda Entertainment Awards 2015 )>>
Akiwa
ni miongoni mwa wanaowania tuzo za MAMA zitakazotolewa mwezi huu,
muimbaji huyo wa ‘Nana’ ametajwa kuwania tuzo zingine za Uganda
zijulikanazo kama Uganda Entertainment Awards 2015 (UEA)
Platnumz
anawania kipengele cha Best African Act akichuana na Wizkid (Nigeria),
Patoranking (Nigeria), Tiwa Savage (Nigeria) na Active
Tuzo
hizo zinatarajiwa kutolewa Septemba 4, 2015 katika hoteli ya Munyonyo
Commonwealth Resort (Speke Ball) jijini Kampala, Uganda.
Thursday, July 2, 2015
Diamond Kuwasha Moto Miss Kilimanjaro>>Soma hapa
Tareheh 24 julai 2015 miss Kilimanjaro inatarajiwa kufanyika katika ukumbi
wa ”KILI HOME MOSHI”ambapo Daimond atawaburuudisha wageni
watakao fika katika ukumbi huo .
Monday, June 15, 2015
Faiza Ally Awaacha Watu hoi Tuzo za Kill 2015>>>SOMA HAPA
Mwanadada faiza ally amezua gumzo kwenye fainali tuzo za
Kilimanjaro music Award zilizofanyika usiku wa kuamkia jana katika ukumbi wa
Mlimani City jijini Dar es salaam.
Mwanadada huyo alitinga kwenye Red kapeti tuzo za kili akiwa
na vazi linao onesha baadhi ya sehemu za makalio zikiwa wazi kama
ambavyo anao onekana katika picha hapo chini suala lililozua minong’ono
kwa baadhi ya watu ukumbini hapo.
Sunday, June 14, 2015
ALI KIBA AONYESHA UBORA WAKE,TAZAMA YOTE YALIYOJIRI HAPA KWENYE TUZO ZA KTMA 2015 NA WASHINDI WOTE>>>
Staa wa filamu za Kibongo, Wema Sepetu 'Beautiful Onyinye' akimtaja mshindi.
Vanessa akiwapagawisha mashabiki wake (hawapo pichani).
MAJINA YA WASHINDI WA TUZO ZA KTMA 20151. KIKUNDI BORA CHA MWAKA - BONGO FLEVA - YAMOTO BAND
2. KIKUNDI BORA CHA MWAKA TAARAB - JAHAZI MODERN TAARAB
3. BENDI BORA YA MWAKA - FM ACADEMIA
4. MSANII BORA CHIPUKIZI - BARAKA DA PRINCE
5. WIMBO BORA WENYE VIONJO VYA ASILI YA KITANZANIA - WAITE -MRISHO MPOTO FT. FELLY KANO
6. WIMBO BORA WA ZOUK/RHUMBA - NITAMPATA WAPI - DIAMOND PLATNUMZ
7. WIMBO BORA WA AFRO POP - MWANA ALI KIBA
8. VIDEO BORA YA MWANAMUZIKI YA MWAKA - MDOGO MDOGO - DIAMOND PLATINUMZ
9.MTAYARISHAJI BORA WA MWAKA BENDI - ENRICO
10. MTAYARISHAJI BORA WA NYIMBO WA MWAKA BONGO FLEVA - NAHREEH
11. MTUNZI BORA WA MWAKA- HIPHOP - JOH MAKINI
12. MTUNZI BORA WA MWAKA BENDI - JOSE MARA
13. MTUNZI BORA WA MWAKA BONGO FLEVA - ALI KIBA
14. MTUNZI BORA WA MWAKA TAARAB- MZEE YUSSUF
Orodha kamili ya washindi wa Kilimanjaro Music Awards 2015........Ali Kiba Kashinda Tuzo 5, Diamond 2>>soma hapa!!
Hii ni orodha kamili ya washindi wa tuzo za muziki Tanzania Kilimanjaro
Music Awards 2015 zilizofanyika 13 June 2015 Mlinani City jijini Dar es
salaam.
1. KIKUNDI BORA CHA MWAKA - BONGO FLEVA - YAMOTO BAND
2. KIKUNDI BORA CHA MWAKA TAARAB - JAHAZI MODERN TAARAB
3. BENDI BORA YA MWAKA - FM ACADEMIA
4. MSANII BORA CHIPUKIZI - BARAKA DA PRINCE
5. WIMBO BORA WENYE VIONJO VYA ASILI YA KITANZANIA (WAITE) -MRISHO MPOTO FT. FELLY KANO
6. WIMBO BORA WA ZOUK/RHUMBA - NITAMPATA WAPI - DIAMOND PLATINUMZ
7. WIMBO BORA WA AFRO POP - MWANA ALI KIBA
8. VIDEO BORA YA MWANAMUZIKI YA MWAKA - MDOGOMDOGO - DIAMOND PLATINUMZ
9. MTAYARISHAJI BORA WA MWAKA BENDI - ENRICO
10. MTAYARISHAJI BORA WA NYIMBO WA MWAKA BONGO FLEVA - NAHREEL
11. MTUNZI BORA WA MWAKA- HIP HOP - JOH MAKINI
12. MTUNZI BORA WA MWAKA BENDI - JOSE MARA
13. MTUNZI BORA WA MWAKA BONGO FLEVA - ALI KIBA
14. MTUNZI BORA WA MWAKA TAARAB- MZEE YUSSUF
15. MTUMBUIZAJI BORA WA MUZIKI WA MWAKA WA KIUME - ALI KIBA
16. MTUMBUIZAJI BORA WA MUZIKI WA MWAKA WA KIKE - VENESSA MDEE
17. MWIMBAJI BORA WA KIUME TAARAB - MZEE YUSSUF
18. MWIMBAJI BORA WA KIUME BONGO FLEVA - ALI KIBA
19. MWIMBAJI BORA WA KIKE TAARAB - ISHA MASHAUZI
20. MWIMBAJI BORA WA KIKE BONGO FLEVA - VANESSA MDEE
21. WIMBO BORA WA TAARAB (MAPENZI HAYANA DHAMANA)- ISHA MASHAUZI
22. WIMBO BORA WA MWAKA (MWANA)- ALI KIBA
23. WIMBO BORA WA KISWAHILI BENDI (WALEWALE) -VIJANA WA NGWASUMA
24. WIMBO BORA WA R&B (SIKSIKII)- JUX
25. RAPA BORA WA HIP HOP - KIPI SIJASIKIA ( PROF J FT. DIAMOND PLATINUMZ)
26. MSANII BORA WA HIP HOP - JOH MAKINI
27. WIMBO BORA WA AFRIKA MASHARIKI (SURA YAKO) - SAUTI SOL
Saturday, June 13, 2015
LICHA YA KUJIFUNGUA UZURI WA AUNT PALEPALE...SHUHUDIA UKWELI HAPA>>
KIWANGO! Tofauti na watu wengine ambaomaumbile yao hubadilika mara baada ya
kujifungua, kwa staa wa sinema za Kibongo,
Aunt Ezekiel hali imekuwa tofauti, uzuri na
umbo lake limebaki vilevile.
Staa wa sinema za Kibongo, Aunt Ezekiel
akiwa na mwanaye.
Akizungumza na wahariri sambamba na
waandishi wa Global Publishers nyumbani
kwake Mwananyamala jijini Dar, Aunt alisema
kilichomfanya asinenepe kupita kiasi na
kuharibika mwili ni mazoezi sambamba na
kufuata ushauri wa vyakula anaopewa hivyo
mwili wake kubaki vilevile.
“Nachukia ubonge nyanya, namshukuru Mungu
pia kwani wengi wakijifungua huwa
wananenepa hovyo lakini kwangu mambo
yamekuwa tofauti. Niko vilevile, nafikiri pia ni
kutokana na kufuata ushauri mzuri wa kula
chakula niliopewa,” alisema Aunt.
Staa wa sinema za Kibongo, Aunt Ezekiel.
Mbali na kutobadilika, Aunt alisema kwa sasa
muda mwingi anautumia kuwa nyumbani na
ubavu wake, Moze Iyobo wakimlea mtoto wao
tofauti na zamani alipokuwa na misele ya
usiku katika viwanja tofauti vya starehe.
Tuesday, June 9, 2015
Dina Marious afunguka ya moyoni, akanusha bifu na Zamaradi >>>
Mtangazji wa redio nchini Tanzania, Dina Marious, baada ya kuwa kimya
bila kusikika katika vipindi vya redio muda mrefu amejitokeza na
kufunguka siri ambazo watu wengi walikuwa hawajui baada ya kuulizwa mara
kwa mara sababu za kutosikika redioni.
Kupitia mtandao wa kijamii amesema “Katika haya maisha hamna kitu
kibaya kama kumuonea na kumnyanyasa mtu ambaye hana hatia.Kwa kutumia
cheo,madaraka,nguvu na nafasi uliyonayo ukiamini huyo mtu hana uwezo wa
kukufanya lolote”.
“Tunaishi katika dunia ambayo binadamu wamekosa utu na imani.Binadamu
wamekuwa wanyama na makatili kuliko wanyama wenyewe.Unaweza ukakutana
na simba na chui porini mkakaa mkatia story lakini sio binadamu”.
“Unafanyiwa unyama eti kisa wanataka revenge kwa mtu wako wa
karibu.Ambae revenge hiyo wala haimuathiri lolote zaidi ni kukutesa wewe
kisaikolojia siku hadi siku. Mbaya zaidi sikustahili miaka yote
nimejituma,nimejitoa,sijawahi kumvunjia heshima alokuwa juu yangu kwa
ngazi zoote”.
“Ndugu zangu nimeishi kwa muda mrefu katika huzuni,msongo wa
mawazo.Na hapa niliponimedevelop na vidonda vya tumbo.Nimekuwa na kitu
kifuani kimenikaaa kila siku nahisi nisiposema nitakufa.Ningekuwa
nimetendewa haki isingeniuma wala kunisumbua ni kwa sababu nimeonewa
sanaa tena katika kipindi kibaya sana”.
“All this time nimekuwa mnyenyekevu na najichekesha nakujitabasamisha
machoni pa watesi wangu.Na wao wakiendelea kunikanyagia chini bila
huruma huku wakinichekea”.
“Leo nimeamka nina huzuni sana sana na ninahuzunika hasa ninapokutana
na msg za kuniuliza niko wapi?mbona sisikiki?? Mimi bado ni muajiriwa
na ninalipwa mshahara ila nimewekwa benchi tu”.
“Kuna kitu naomba nikiweke clear kumekuwa na maneno mengiiiiii
yanazunguka kuwa nina ugomvi na Zamaradi.Mimi sina ugomvi na Zamaradi
sijui ndio amechangia mimi kutolewa kwenye leo tena.Thats not true wala
nguvu hiyo hana.Sijajua why watu husema hivyo ila sina ugomvi nae.Hata
yeye anajua hatuna ugomvi wowote.Nilipotoka pale niliamua kubadili mfumo
wangu wa maisha hivyo hatuna ukaribu kama zamani.Ila haimaainishi tuna
ugomvi”.
“Na malizia kwa kusema sipo radio wala sipo tv kwa sasa.Maswali
mnaniuliza kila siku na nina wajibu kila mara na leo nimewajibu
tena. ila nitakuwa kwa radio na tv hapo baadae acha niuze mafuta ya
nazi.Maelezo ya mwanzo yamejitosheleza sanaa na sitaenda mbalii sanaa
labda nikiandike kitabu ndio yatatimia”.
“Nimeandika haya kwa ufupi mjue hata sisi pamoja na majina tuliyonayo
changamoto zipo na tunakabiliana nazo.Na ipo siku tutashinda maana
mtetezi wetu yu hai”.
Monday, June 8, 2015
Tuesday, June 2, 2015
Sunday, May 31, 2015
DIAMOND PLATNUM AJIPALILIA TUZO KAMA CHRISTIAN RONALDO.
Home
» KIMATAIFA
» MATUKIO
» MICHEZO
» WASANII
» DIAMOND PLATNUM AJIPALILIA TUZO KAMA CHRISTIAN RONALDO.
DIAMOND PLATNUM AJIPALILIA TUZO KAMA CHRISTIAN RONALDO.
Wednesday, May 27, 2015
Wema Sepetu msamehe Kajala-Mashabiki
Ni Siku moja tu imepita toka msanii wa filamu nchini Kajala
Masanja kufunguka ya moyoni juu ya Wema Sepetu na Petit Man na kueleza
kuwa kamwe katika maisha yake ya hapa Duniani hawezi kusahau fadhila na
moyo wa upendo ambao ulioneshwa
na watu wao kipindi ambacho alikuwa na matatizo na jinsi walivyoweza
kujitolea mpaka kufikia hatua ya kuweza kumsaidia katika matatizo ambayo
alikuwa anakabiliana nayo kwa kipindi kile.
Kajala alifunguka hayo kupitia ukurasa wake wa Instgram na ndipo hapo
alipoamsha hisia za mashabiki ambao wameanza kumuomba Wema Sepetu
kumsamehe Kajala ili waweze kumaliza tofauti zao ambazo wanazo sasa.
"Binadamu tuliumbwa kuishi katika misingi ya ubinadamu na sio unyama kama waishivyo wanyama wa porini leo naomba kusema kutoka moyoni mwangu.. najua kabisa nina wazazi wangu ndugu zangu na zaidi sana mungu wangu ila kuna watu mpaka nakufa kamwe sintowasahau katika kuta za moyo wangu katika kipindi changu kigumu nilichopitia mlikuwa nembo na mboni kubwa katika kuokoa maisha yangu..
"Napenda kusema kuwa hata kwa haya yote tunayopitia bado ni madogo sana kuficha thamani yenu mliyoijenga juu yangu..nakumbuka sana mlipojitoa kwa ajili yangu mlipojinyima kwa ajili yangu mlipopigana kwa ajili yangu, mlivyofedheheka kwa ajili yangu yote hayo nayakumbuka na namshukuruu mungu kwani naona kabisa mliletwa duniani kwa sababu nyingi na moja ya sababu ilikuwa kuniokoa katika kipindi kigumu katika maisha yangu.
"Leo hii tarehe 25.5.2015 napenda kusema kwa Umma na zaidi kwa mungu wangu kuwa nawathamini nawapenda na nashukuruuu sana kwa yote mliyofanya juu yangu.. nawaombea kwa mungu muendelee na moyo huo huo kwani naamini kuna wengi bado wanawategemea ili kukomboa maisha yao kwa wakati aliyopanga Mungu. hata kitabu cha dini kilisema kuwa "huwezi kumpenda mungu usiyemuona wakati unamchukia ndugu yako unayemuona" najua siku moja tutaishi kama zamani.." Aliandika Kajala
Baadhi ya mashabiki wameonesha kupenda jambo ambalo limefanywa na Kajala na kuona kuwa amefanya jambo la kiungwana sana na anastahili pongezi au msamaha kama kweli kuna jambo alitenda ambalo ndilo limeleta utofauti wao ndiyo maana mashabiki hao wamemtaka Wema Sepetu na Martin Kadinda kuweza kumsamehe ili waweze kuishi kama ambavyo walikuwa wakiishi mwanzo.
"Mwantumum Kilindi: Good sana my Kajala nimeipenda Allah atawasaidia mtaishi kama zamani mwenyezi Mungu kasema mara saba sabini na inapendeza binadam kushirikiana si unafiki binadamu haipendezi kununiana maana kila binadamu ataoza leo hii usimchukie binadamu mwenzako kwa kosa gani haswa lisilo sameheka minatafurahi endapo mtapatana wote na Aunt Wema na wewe Kajala ila marafiki sikuzote si wakumueleza undani wako namkishakua marafiki wa tatu ni unafiki utaendelea nawapenda wote, sote tutafukiwa hujui nani atatangulia leo hata kesho allah atawaongoza."
"Irene.Kimenye: Binadamu wote ndugu mlisahau kabisa kwamba ninyi ni kioo cha jamii nakumbuka kwenye kipindi cha mkasi ulichohojiwa ulikiri Wema ndiye aliyekufundisha biashara na mambo ya mtandao. Urafiki wenu watu wengi nikiwemo mimi niliupenda lakini haukufika popote mlichogombana mnakijua ninyi.Kama umekaa na ukafikiria na ukaona haya uliyoyaandika hakika Mungu atawaongoza na mtarudi kama zamani ingawa sio kwa ukaribu ule.
"Emelinaswebe: Wema msamehe mwezio jamani,haya ni maisha tu yanapita, mnabidi mmalizane"
"Jasleeee_ safi sana Kajala Mungu ni mwema siku zote amini kila jambo linasababu kwa Mungu. amini utayaweza yote katika yeye akupae uzima. hivyo iko siku wema atakusamehe na mtaendelea kama zamani kwani hizo nitofauti tu za kawaida mpendwa."
"Ajumysalum: Jamani huu ndiyo ungwana Kajala hongera sanaa @wemasepetu @new_kajala samehaneni bhana asante @ my shoga @pendojerry for the tag imenifunza kitu hii

Monday, May 25, 2015
NAJUTA KUBALEHE...NI STORY MPYA SOMA HAPA>>>>
SEHEMU YA 01
mwaka 2007 tulihama kutoka kijijin na kuhamia ndan ya mji wa arusha. nikiwa na miaka 14 haki ya mungu arusha ni jiji zuri sana lina manzari nzuri basi pale tulipofikia palikua na wasichana jiran weng sana. kwaharaka ckuelewa kwann eneo lile lina warembo weng sana ikiwa ndo mwanzo wa balehe muda mwingi hisia za ngono zilitawala ubongo wangu.
kibaya zaid skuwah kusex zaid ya enz za utoto nikiwa nina wiki moja tangia tuhamie arusha maeneo ya mianzini. jion moja kijana prince niliamua kumvizia mdada fulan. nikajibanza chocho mara nikamuona anakuja nikaanza kutetemeka huku nikiwaza nitasemaje.
nikiwa naendelea kuwaza mara mtoto akanifikia akabidi nijikaze kiume "dada samahan naweza kukusemesha"akajibu"bila shaka nakusikiliza ongea kijana" nikajua hapa mambo sio mabaya "dada mimi naitwa prince hapa si mwenyeji sana kwanza ndo juz tu tumehamia mtaani hapa "akacheka kidogo kisha akasema "nashukuru kukufaham prince unajina zuri sana mm naitwa hidaya "
ITAENDELEA

Jokate Amtolea Uvivu Diamond Baada Ya Kumuita MAKOMBO
Sexy lady anayefanya poa na ngoma yake ya Leo Leo, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’, amemlipua aliyewahi kuwa mwandani wake, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ ambaye hivi karibuni alimwita makombo baada ya kusikia kwa sasa anatoka kimalovee na msanii Ali Kiba.
Akizungumza na gazeti la Ijumaa Wikienda,, Jokate alisema alishangazwa na maneno hayo ambayo
hakustahili kuyatamka kwani kama ni ishu ya mtu kula makombo mbona hata
yeye ni makombo na bado anakula makombo?
“Sijapendezwa na kauli ya Diamond na namshangaa sana, sijajua nini
kimemkuta maana mimi sijamtaka wala hakuna ambapo niliwahi kumwambia
kuwa ninatoka au ninamtaka Kiba, zaidi ya maneno ya watu kwenye
mitandao ya kijamii.
“Hata kama hilo lipo, bado sioni maana ya neno makombo kwani hata
yeye ni makombo na anakula makombo kwa Zari (Zarinah Hassan) kwani nani
asiyejua?” alihoji Jokate akionekana kuchukizwa na kauli hiyo ya Diamond
na kuongeza:
“Yawezekana labda maana ya neno hilo hatulijui ndiyo maana tunalisema
bila kuliangalia kwa umbali zaidi, hivyo ninachoweza kukisema ni kwamba
mimi sijawahi kumtaka wala kumhitaji hivyo sioni kabisa sababu ya
msingi ya kusema hivyo labda kama alikuwa na maana nyingine tofauti na
hiyo.”Credit: Gazeti la Ijumaa/Gpl
Sakata la Picha Za UCHI......Shilole Awaomba Radhi Wanawake Kwa Kuwadhalilisha
Baada ya wiki kadhaa
kupita tangu picha zake zisambae zikimuonesha gauni likiwa limevuka
nakuachia maziwa wazi, staa wa Bongo Fleva, Zuwena Mohamed ‘Shilole’
ameibuka na kuwaomba radhi kinamama wote.
Shilole
amesema kuwa anajua kwamba kitendo hicho kimewakwaza wengi na
hakukusudia kufanya jambo kama lile.
“Nimejifunza mengi na naendelea tena kuomba msamaha kuwa tatizo hili halitajitokeza tena ,niwaombe radhi kina mama na mashabiki wangu,” alisema.
Shilole alifanya tukio hilo alipokuwa jijini Antwepen, Ubelgiji kwenye shoo ambapo aliongozana na mpenzi wake,Nuh Mziwanda.

Subscribe to:
Posts (Atom)