
Showing posts with label Waigizaji. Show all posts
Showing posts with label Waigizaji. Show all posts
Wednesday, June 14, 2017
Monday, July 25, 2016
Thursday, July 21, 2016
Saturday, July 4, 2015
Jose Chameleone aahidi kumpiga jeki Wema kwenye safari yake ya kuwania ubunge>>
Jose Chameleone yupo tayari kumsaidia Wema Sepetu kwenye harakati
zake za kuwania nafasi ya ubunge wa viti maalum mkoani Singida.
Petit ambaye ni mmoja wa watu walio karibu na Wema amepost screeshot
kwenye Instagram ya mazungumzo na Chameleone kwenye WhatsApp.
“S/O to my bro Jchameleone kwa kuonesha support pale inshallah
atakapochukua mama form ya kugombea Ubunge Viti maalum.. Tutakuwa nae
kwenye campaign mwanzo mwisho.. Thank u so much bro.. Lets support Wema
Sepetu,” aliandika Petit kwenye picha hiyo chini:
Saturday, June 27, 2015
Wema Sepetu Amtaja Mtu Anayemzuia Kupata Mimba>>
Ishu ya Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu kutopata ujauzito imeshazungumzwa mara kadhaa na hata yeye mwenyewe alishawahi kujitokeza na kuizungumzia lakini safari hii amelizungumzia kwa njia tofauti.
Wema ambaye pia ni muigizaji wa filamu,
awali alisema sababu kubwa ya kutopata ujauzito ni masuala ya kiafya
lakini safari hii ametoa kauli tata ambayo inahusiana na imani za nguvu
za giza.
Wema ambaye alifunguka hayo hivi karibuni, anadai kuwa yawezekana marehemu Steven Kanumba anahusika kwenye suala hilo.
Mizimu ya Kanumba
“Unajua hili suala la mtoto linanisumbua
sana yaani na linaniuma kwa sababu napenda watoto sana na pia napenda
kuitwa mama, nimehangaika sana katika kuhakikisha nafanikiwa katika hili
lakini ndiyo hivyo imeshindikana.
“Serious! Ilifika kipindi yaani nilikuwa
nachukia nilipokuwa nikiziona siku zangu, nilikuwa sipendi kukutana na
hiyo hali kwa sababu naumia sana lakini ndiyo hivyo baada ya kuhangaika
sana inabidi nimwachie Mungu tu. Nahisi kukata tamaa lakini bado
sijakata tamaa.
“Watu wananiambia mimi bado mdogo kwa
hiyo sitakiwi kuwa na wasiwasi sana ila muda unakwenda, sasa nina miaka
27. Niliwahi kupata mimba mwaka 2008, aliyenipa alikuwa marehemu
Kanumba, lakini baadaye ilitoka na aliposikia hivyo (Kanumba)
alikasirika kwa kweli.
“Lakini baadaye ikawa kawaida, hata
nilipokuja kuachana naye, bado alikuwa rafiki yangu na tulikuwa
tunaongea vizuri na kupigiana simu kama kawaida ila alikuwa ananiambia
‘unajua una deni, nakudai watoto wangu na nitafanya juu chini ili
unilipe’.
“Basi ikawa kawaida yake kuniambia
hivyo, wiki chache kabla ya kufariki aliniomba tuonane lakini
haikuwezekana kutokana na ratiba zetu kutofautiana.
“Kuna muda huwa nafikiri au mizimu yake inahusika katika hii ishu! (anacheka sana).
“Unajua ile mimba ya Kanumba hata mimi
sikuwa tayari kupata mtoto wakati ule, niliona ndiyo kwanza naingia
kwenye mapenzi halafu ndiyo nimetoka kuwa miss tu, sasa itakuwaje,
lakini huwezi jua labda pengine kwenye ‘abortion’ walivuruga baadhi ya
vitu ndiyo maana mpaka leo imekuwa hivi.”
Ujauzito wa Zari
Wema ambaye pia aliwahi kuwa na uhusiano
wa kimapenzi wa ‘on-off’ na msanii Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’,
anafunguka juu ya ujauzito wa mpenzi wa sasa wa Diamond, Zarinah Hassan
‘Zari The Boss Lady’.
“Unajua hiyo mimi hainisumbui, sababu
nilishakubali kwamba sasa nimeachana na Nasibu kwa hiyo ishu nyingine
zote ziko poa. Najua jinsi gani alivyokuwa anatafuta mtoto, namtakia
kila la kheri.”
Gari alilopewa na Diamond
“Ile Murano niliiuza kwa kuwa ilikuwa
mbovu na sikuwa naipenda kwa sababu ilikuwa inanisumbua, niliamua hivyo
kwa kuwa lilikuwa langu.”
Saturday, June 20, 2015
Kadinda: Wema Anachangamoto Hii Kwenye Siasa
Meneja wa Wema Sepetu, Martin Kadinda amesema anaamini kuwa muigizaji huyo anaweza kuwa kiongozi mzuri japo changamoto inayomkabili ni kubadilisha mawazo ya watu juu yake hasa kutokana na maisha yake ya ustaa na mapenzi.
Martin ameiambia Bongo5 kuwa kinachotakiwa sasa ni kuwabadili watu waanze kumchukulia kama mwanamke anayeweza kuwa kiongozi.
“Watu wengi wametokea kumsupport kwa sababu walikuwa wanamsikia baba yake akimtaka aingie kwenye siasa, na wengine walikuwa wanamtaka Wema aingie kwenye siasa,”amesema Martin.
“Lakini ana kazi kubwa ya kuweza kubadilisha watu jinsi wanavyomchukulia. Kwahiyo anachukulia positive kwa sababu watu aliokuwa nao wameweza kumsupport. Lakini kabla hatujafika huko sasa tutamuona kama kiongozi sioo kama msichana wa bongo movie. Tumuamini Wema kama anaweza kuonyesha tu nia hata asipopata tukumbuke kuonyesha nia tu ni kupata, kwa sababu ana ndoto kubwa sana anataka kuzifanya,” ameongeza.
Hivi karibuni Wema alitangaza nia ya kuwania ubunge wa viti maalum kwa tiketi cha chama cha mapinduzi mkoani Singida.
Bongo5
Picha: Wema Sepetu akiwa na petitman
Subscribe to:
Posts (Atom)



