Serikali ya Burundi imetangaza kuwa uchaguzi wa rais na wabunge
uliotarajiwa kufanyika Ijumaa hii umehairishwa mpaka tarehe nyingine
itakapopangwa.
Msemaji wa rais Nkurunzinza,Wily Nyamitwe amesema kuwa tarehe itapangwa na wasimamizi wa uchaguzi wa nchi hiyo.
Mabadiliko hayo yamekuja kutokana na taifa hilo kuingia kwenye
machafuko tangu Rais Piere Nkurunzinza kutangaza nia ya kuongoza kwa
awamu ya tatu baada ya kuwa rais kwa miaka 10.
Umoja wa Mataifa imeelezea jinsi mgogoro huo ulivyoongeza idadi ya wakimbizi wanaoikimbia Burundi na kukimbilia nchini Tanzania.
Hata hivyo umoja wa Afrika mashariki unadaiwa kushindwa kutoa amri
dhidi ya Rais Nurunziza kutokana na kutaka kujiongezea muda wa kukaa
madarakani kinyume na katiba ya nchi hiyo suala linalopingwa vikali na
wananchi wa nchi hiyo.
0 comments:
Post a Comment