Mbunge
wa Tarime Vijijini, John Heche amefunguka na kusema kwa kuwa Rais
Magufuli kupitia ripoti ya pili ya mchanga amesema kampuni ya ACACIA ni
feki na haipo basi yeye anawaambia wananchi wa jimbo lake wajiandae
kuingia mgodini kuchukua kila kitu.
Heche
amesema hayo bungeni jana na kudai kuwa atasimamia zoezi hilo na
kuhakikisha kuwa ndege za kampuni hiyo zikitua mgodini kwa ajili ya
kubeba madini basi zinapigwa mawe kwa kuwa wananchi wa jimbo lake la
Tarime ambapo hiyo migodi ipo wameumizwa sana kusikia hiyo kampuni
inayochukua mali zao ni feki na hewa.
"Kampuni
ile ya ACACIA Rais amesema feki na hakuna 'formula' ya kukamata mwizi
mlisema wenyewe, formula ya kukamata mwizi ni kupambana naye sisi
hatutaruhusu madini yatoke pale ndege ikitua itapigwa mawe, magari yao
tutayakamata kwanza tunawadai fidia nyingi kweli kweli pale Tarime.
"Mhe.
Spika sisi tulitegemea Mhe. Rais aseme madini yasiondoke nchini mpaka
mambo hayo yote yapitiwe, tutazuia mchanga madini yanaondoka.
"Rais
amesema ACACIA ni mwizi wewe unataka utaratibu wa kukamata mwizi
Tarime, sisi watu wetu wameumia sana na maji ya sumu, ng'ombe wamekufa,
watu wamepigwa risasi kwa mujibu wa ripoti ya Waziri wa Nishati na
Madini watu wa Tarime zaidi ya 64 wameuawa pale mgodini" alisema Heche
Mbali
na hilo John Heche alisema kuwa kama serikali itamkamata kwa maamuzi
ambayo atafanya basi Watanzania watajua kuwa serikali haipo tayari
kupigana vita hii ya kupigania rasilimali za nchi hii, hivyo amewataka
watu wa jimbo la Tarime wajiandae na kuanza maandalizi ya kupigania
rasiliamali zao ili waone kama serikali itapeleka jeshi la polisi
kulinda mali za wezi hao.
==>Msikilize Hapo chini akiongea
==>Msikilize Hapo chini akiongea
SAWA
ReplyDelete