MBUNGE
wa Viti Maalum, Christowaja Mtinda (Chadema), ameitaka Serikali kutunga
sheria itakayoilazimisha mifuko ya hifadhi za jamii, kuwakata moja kwa
moja wanachama wake wanaodaiwa na Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu.
Akiuliza
swali la nyongeza bungeni jana, Mtinda alisema kwa sasa mifuko huyo
haitaki kuwakata wadaiwa hao kwa kuwa sheria zilioanzisha mifuko hiyo
haziruhusu kuwakata moja kwa moja.
“Kwa
nini sasa Serikali isilete muswada wa sheria ya kuilazimisha mifuko
hiyo kushirikana na Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu kuwakata wanachama
wanaodaiwa na bodi hiyo ili mikopo hiyo iweze kurudishwa kwa wakati?”
alihoji.
Akijibu
swali hilo, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa
alisema kwa sasa Bodi ya Mikopo huipatia mifuko hiyo majina ya wadaiwa
sugu.
“Hata hivyo Serikali ipo katika mchakato wa kuandaa muswada wa sheria kuhusiana na masuala hayo,” alisema.
Awali
akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Catherine Magige (CCM), Dk.
Kawambwa alisema jumla ya mikopo yenye thamani ya Sh. trioni 1.8 kwa
wanufaika 2191,582 katika kipindi cha mwaka 1994/95 hadi 2013/14.
“Hadi
Aprili 30, mwaka huu mikopo ya Sh. bilioni 70.83 ilikuwa imerejeshwa
kutoka kwa wanufaika 136,803 kati ya wanufaika 177,017 ambao mikopo yao
imeiva.
“Wanafunzi
40,819 ambao hawajaanza kurejesha mikopo, Bodi imeanza kuwachukulia
hatua mbalimbali ili wawezse kurejesha,” alisema.
Alisema
hatua hizo ni pamoja na majina yao kutangazwa kwenye vyombo vya habari,
baadhi wameanza kushitakiwa mahakamni, kuzuiwa kupata udhamini katika
masomo ya elimu ya juu ndani na nje ya nchi na waajiri wa wanufaika wa
mikopo hiyo wameanza kushitakiwa mahakamani.
“Mei 21 mwaka 2013, Bodi iliwafungulia kesi mahakamani wadaiwa 18 wasiolipa mikopo yao katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
“Kati
ya hao, wadaiwa watano waliamuliwa kulipa madeni yao pamoja na faini
wakati wengine 13 kesi zao zinaendelea kusikilizwa,” alisema.
Aidha, Dk. Kawambwa alisema Bodi ilifungua kesi kwa waajiri watatu waliokaidi kutoa taarifa dhidi ya watumishi wao wanaodaiwa.
Katika
swali lake Magige alitaka kujua idadi ya wanafunzi walionufaika na
mikopo, idadi ya waliorejesha na hatua zilizochokuliwa kwa waliogoma
kurejesha.
0 comments:
Post a Comment