SERIKALI imesema kati ya viwanda 131 vilivyobinafsishwa ni viwanda 90 tu ambavyo vinafanya kazi.
Taarifa
hiyo ilitolewa bungeni jana na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara,
Janeth Mbene wakati akijibu swali la Mbunge wa Ileje, Aliko Kibona
(CCM).
Katika
swali lake Kibona alitaka kujua mpango wa Serikali wa kufufua viwanda
vilivyokufa Mkoa wa Mbeya na mikoa mingine ili kukabiliana na tatizo la
ajira nchini.
Mbene alisema viwanda 41 vilivyobinafsishwa vimefungwa kutokana na sababu mbalimbali.
“Kwa
viwanda vilivyofungwa, wizara imewasiliana na ofisi ya Mwanasheria Mkuu
wa Serikali ili watoe maoni kwa mujibu wa maktaba wa viwanda vyao.
“Nia
ni kupata ushauri wa namna bora ya kuvifufua ikiwa ni pamoja na
kuvitwaa na kuvirejesha Serikalini pale ambapo itaonekana ndiyo njia
sahihi ili Serikali itafute mwendelezaji mwingine,” alisema
Alisema
wizara yake kupitia Shirika la Viwanda Vidogo (SIDO), imepatiwa eneo na
Halmashauri ya Ileje kwa ajili ya kujenga viwanda vidogo vya kusindika
nafaka, kutengeneza maji ya kunywa, kiwanda cha biskuti na mafuta ya
kula.
Mbene
alisema mara taratibu zitakapokamilika, Halmashauri hiyo itawakaribisha
wawekezaji wa viwanda vidogo ambavyo vitawezesha Wilaya ya Ileje na
Mkoa wa Mbeya kwa ujumla kukua kiuchumi.
Mpekuzi blog
0 comments:
Post a Comment