JUMLA ya silaha 136 kutoka kwa wananchi zilikamatwa wakati wa Oparesheni Tokomeza.
Taarifa
hiyo ilitolewa bungeni jana na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Pereira
Silima wakati akijibu swali la Mbunge wa Manyoni Mashariki, John
Chiligati (CCM).
Katika
swali lake Chiligati alitaka kujua idadi ya silaha zilizokamatwa wakati
wa oparesheni hiyo na lini wamiliki halali wa silaha hizo
watarudishiwa silaha zao.
Silima
alisema silaha zilizopatikana na kuhifadhiwa katika vituo vya polisi
wakati wa zoezi hilo ni pamoja na shortgun 16, bastola moja, Riffle 16
na magobore 114.
“Uchunguzi
wa awali ulionesha kuwa kati ya silaha 136 zilizokamatwa ni silaha 16
tu yaani Riffle 4 na Shortgun 12 ndizo zinamilikiwa kihalali, silaha
zilizobaki zinaendelea kufanyiwa uchunguzi na Jeshi la Polisi kuhusiana
na matukio mbalimbali ya kiuhalifu,” alisema.
Silima
alisema kuhusu zoezi la kuwarejeshea wamiliki silaha zao itategemea
matokeo ya kesi zilizopo mahakamani na uhakiki unaofanywa na polisi
utakapokamilika.
0 comments:
Post a Comment