MBUNGE
wa Viti Maalum, Amina Abdallah Amour (CUF) ameitaka Serikali kueleza
imefaidikaje na ujio wa Rais wa Marekani, Barrack Obama mwaka 2013.
Akiuliza
swali bungeni jana, Mbunge huyo alisema mwaka 2013 Tanzania ilipata
ugeni huo wa Rais wa Marekani na kutaka kujua faida za kisiasa na
kiuchumi kutokana na ujio huo.
“Je Taifa limefaidika vipi kisiasa na kiuchumi kutokana na ujio wa kiongozi huyo mkubwa duniani?” alihoji.
Akijibu
swali hilo, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Mahadhi Juma Maalim alisema
akiwa Tanzania Obama alitangaza mpango wa Serikali yake wa kusadia
miradi ya umeme ujulikanao kama Power Initiative.
“Kupitia
mpango huo, Serikali ya Marekani imetenga Dola za Marekani bilioni 7
wakati wa sekta binafsi nchini Marekani imetenga Dola bilioni 9,”
alisema.
Alisema
pia katika kupambana na ujangili, Serikali ya Marekani imetoa vifaa
vya mafunzo na mafunzo ya kujenga uwezo wa wataalamu.
“Machi 2015, Marekani ilitoa msaada wa vitabu milioni 2.5 vyenye thamani ya Dola za Marekani milioni 5.5.
“Kupatikana
kwa vitabu hivyo kumesaidia kupunguza uhaba wa vitabu vya masomo ya
sayansi na kupunguza uwiano wa upatikanaji wa vitabu kwa wanafunzi,”
alisema.
Alisema
ziara za viongozi wakuu wa nchi ni njia mojawapo muhimu ya kukuza
urafiki na uhusiano baina ya Tanzania na nchi nyingine.
0 comments:
Post a Comment