VIONGOZI
wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wanatarajia kukutana kesho Jijini Dar es
Salaam kwa ajili ya kujadili msimamo wa Burundi wa kuendelea na
uchaguzi wakati bado nchi hiyo ipo kwenye machafuko.
Taarifa
hiyo ilitolewa bungeni jana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa, Bernard Membe wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum,
Dk.Mary Mwanjelwa (CCM).
Katika
swali lake Dk. Mwajelwa alitaka kujua msimamo wa Tanzaniua kuhusu
uamuzi wa Burundi kuendelea na uchaguzi Juni 26, mwaka huu, licha ya
kuwepo kwa machafuko.
Mbunge huyo alisema machafuko hayo yamesababisha wakimbizi zaidi ya 51,000 kuingia nchini na kuisababisha nchi hasara.
Membe
alisema ni kweli baada ya machafuko kutokea Mei 6 mwaka huu na jaribio
la kutaka kumuondoa madarakani Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza,
Rwanda ilipokea wakimbizi wasiopungua 150,000 na Tanzania ilipokea
wakimbizi 51,000.
“Wakimbizi hawa waliingia kwenye maeneo yetu na kusababisha uharibifu mkubwa hasa kwenye shule za msingi, mazao na mifugo.
“Hali hii imesababisha Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Dk. Jakaya Kikwete kushughulikia utatuzi wa suala hili.
“Kuhusu
suala la uchaguzi wa Juni 26 mwaka huu Viongozi wa Afrika Mashariki
wanakutana keshokutwa (kesho) Dar es Salaam ili kulishughulikia tatizo
la usalama na hali ya uchaguzi nchini Burundi,” alisema.
Membe alisema msimamo wa Tanzania ni kwamba wanaitaka Burundi na hasa Warundi watulie wayamalize matatizo yao ndani.
“Jumuiya ya Afrika Mashariki itakuwa tayari kuwasaidia kuondokana na tatizo hili ambalo linatuletea wakimbizi nchini.
“Tanzania
tunaamini amani ya Burundi ni amani ya Tanzania kwa hiyo tutawasaidia
kwa lolote lile ili kuhakikisha amani ya Burundi inarejea,” alisema
Membe.
0 comments:
Post a Comment