Pages

Ads 468x60px

Friday, June 19, 2015

ANTHONY MAVUNDE:MKUU WA WILAYA ALIYEANZA NA MABADILIKO MAKUBWA MPWAPWA...CHEKI ALICHOFANYA HAPA

 
Picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Huduma za Maktaba Ndg Alli A.S.Mcharazo katika ofisi za Maktaba ya Taifa baada ya kuwasilisha maombi ya vitabu vya kiada na ziada kwa shule za Sekondari na Msingi wilaya ya Mpwapwa.
Maombi yetu yamekubaliwa na Wilaya ya Mpwapwa itapatiwa vitabu husika ndani ya muda mfupi ujao.
Aidha pia tumekubaliana kwa pamoja juu ya uanzishwaji wa Maktaba katika wilaya ya Mpwapwa ili kutoa fursa kwa wanafunzi na wananchi wa Mpwapwa kujiongezea maarifa kupitia usomaji.
BODABODA MPWAPWA
Tumefanya mazungumzo na Kampuni ya T & J GROUP LIMITED kwa lengo la kusaidia upatikanaji wa pikipiki kwa njia ya mkopo kwa Vijana na watumishi wa serikali waliopo wilayani Mpwapwa.
Tumekubaliana na kampuni hii waje Mpwapwa wiki ijayo kwa lengo la kujitambulisha na kutoa muongozo wa upatikanaji wa mikopo hiyo ili tuanze utekelezaji.
Hizo ni baadhi ya kazi alizofanya DC mpya wa wilaya ya Mpwapwa Bw.Anthony Mavunde ikiwa ni kujaribu kuwaletea maendeleo wananchi wa mpwapwa...Masama Blog inamtakiakila la heri Mkuu huyu wa wilaya ya Mpwapwa...

0 comments:

Post a Comment

SHARE