KAMPUNI
ya Bima ya Zurich Brokers (EA) Ltd imeanza mchakato wa kuwaondoa
waendesha bodaboda jijini Mwanza katika bima ndogo ya Sh 10,000 hadi Sh
125,000.
Akizungumza
Mwanza juzi, Meneja wa Zurich Insurance Broker (EA) Ltd, Kanda ya Ziwa,
Curtis Mukami, alisema wameamua kumsafirisha kiongozi mmoja wa bodaboda
hadi Dar es Salaam ili kufanya mazungumzo ya kuwasaidia kukata bima ya
Sh 125,000.
Alisema
kampuni yao imepokea taarifa ya bodaboda hao jinsi wamiliki wa pikipiki
wanavyokata bima ndogo ambayo haiwasadii pale wanapopata ajali au
tatizo lolote.
“Tunapozungumza
hapa, Mwenyekiti wa Shirikisho la Machinga Manispaa ya Ilemela, Dennis
Nyamlekela yupo Dar es Salaam, viongozi wetu wa kitaifa watakaa na
wauzaji wa pikipiki, bajaji, magari ili kuweka mkakati wa pamoja na
kuwaokoa madereva.
“Tunataka
kila mwendesha pikipiki, mmiliki pamoja na mtu atakayekuwa ameguswa kwa
namna yoyote na ajali au tatizo la chombo hicho alipwe, lakini kama
dereva hatakuwa na leseni na kwa bahati mbaya akapata ajali, hapo
hatalipwa, hivyo hivyo na mmiliki,” alisema Mukami.
Naye
Ofisa Huduma kwa Wateja wa Zurich, Hyasinta Tarimo, alisema Watanzania
wengi wamekuwa wakikata bima ya moto kwa ajili nyumba zao, lakini
wanashindwa kutambua kuna bima ya wizi na majanga, yakiwamo mafuriko.
Alisema asilimia 98 ya Watanzania wanaomiliki nyumba zao hawana bima ya mali zao zilizomo ndani ya nyumba na majanga.
Alisema
baada ya kampuni hiyo kuzinduliwa Mwanza, kumekuwapo na mwitikio mkubwa
wa wamiliki wa pikipiki, magari, nyumba na afya na kwa mwezi mmoja
wamefanikiwa kupata wanachama zaidi ya 400.
“Kikubwa
tunawaomba wamiliki wa shule binafsi, vyuo, madhehebu, hospitali kukata
bima ili kuweka mali zao salama, baada ya kuzinduliwa kampuni yetu,
tumebaini watu hawana uelewa wa bima isipokuwa wale watumishi wa umma na
mashirika,” alisema Tarimo.
0 comments:
Post a Comment