1.Kesi ya Kulawiti:
KESI
ya kulawiti inayomkabili Mwenyekiti wa Chama Cha Mapindizi (CCM) wilaya
ya Uyui mkoani Tabora, Mussa Ntimizi, imeahirishwa hadi Juni 26 mwaka
huu itakapotajwa tena.
Wakili
wa Serikali, Juma Massanja, alisema kesi hiyo imeahirishwa kutokana
na kutohudhuria mashahidi wa upande wa mashtaka. Ilisomwa juzi mbele ya
Hakimu Jocktan Rushwera.
Mwisho
-------
2.Kesi ya vigogo Julai 21
KESI
inayowakabili vigogo watatu wa Serikali ya matumizi mabaya ya madaraka
na kutumia vibaya nyaraka mbalimbali kumtapeli mwajiri wao, jana
iliahirishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Nyamagana hadi july 21.
Vigogo
waliofikishwa mahakamani jana ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya
ya Msalala Mkoa wa Shinyanga, Patrick Karangwa (45), Mkurugenzi wa
Halmashauri ya Wilaya ya Magu Mkoa wa Mwanza, Ntinika Paul (51) na
Mhasibu Mkuu wa Wilaya ya Magu, Mathayo Masuka.
MWISHO
3.Jeshi Latoa Elimu kwa wananchi
JESHI
la Polisi mkoani Mwanza limeamua kutoa elimu kwa wananchi wa Kata ya
Kishiri iliyopo wilayani Nyamagana kwa lengo la kuacha kujichukulia
sheria mkononi.
Hatua
ya jeshi hilo kutoa elimu imetokana na vitendo vya wananchi wa eneo
hilo kujichukulia sheria mikononi ambako hivi karibuni polisi PC
Magesa aliuawa na wananchi kwa kile kilichodaiwa alikuwa amekusudia
kuiba mafuta kwenye minara.
0 comments:
Post a Comment