MKURUGENZI
Mkuu wa Shirika lisilo la Serikali linalojishughulisha kutetea haki
za watu wenye albinism la Under The Same Sun (UTSS) ,Peter Ash,
ameupongeza Umoja wa Mataifa kwa kuitangaza June 13 kila mwaka kuwa siku
ya watu wenye ulemabu wa ngozi duniani.
Akizungumza
hivi karibuni katika ibada maalumu ya kumshukuru Mungu kwa siku ya
uelemavu wa ngozi duniani iliyofanyika Kanisa la Tanzania Assemblies
of God Beacon Mission Christian Centre, lililoko Mtaa wa Nyamalango
Saut Malimbe jijini Mwanza na kuhudhuriwa na baadhi ya wafanyakazi wa
UTSS, akiwemo Mkurugenzi Mtendaji, Vicky Ntentema, Ash alisema hiyo
ni hatua muhimu iliyofikiwa.
Alisema
amefurahishwa na Umoja wa Mataifa kuitangaza siku hiyo kwa kuwa
anaamini ni hatua nzuri ambayo itasaidia watu wenye ulemavu wa ngozi
nchini na duniani kote kupata nafasi ya kujadiliwa haki zao na mataifa
mbalimbali.
“Niko
hapa kanisani kwa sababu tangu kuibuka kwa mauaji na ukatwaji viungo
kwa watu wenye ulemavu wa ngozi Tanzania, nimekuwa nikimuomba Mungu kila
siku ili atusaidie na mauaji haya siku moja ibaki historia,watu
wanadhani kwamba kwenda kanisani na kutoa sadaka nyingi ndiyo kumcha
Mungu , hawajui kuwa kanisa sio chama cha wakristo bali ni mahali pa
watu wanaohitaji huruma, wema na upendo.
“Niko
hapa leo kwa ajili ya kuwahudumia walio na uhitaji watu wenye ulemavu
wenzangu ambao wanatekwa, wanakatwa viungo vyao wanatemwa mate na
kuuawa, Mwenyezi Mungu anataka mambo matatu tu kutoka kwetu wanadamu
ambayo ameyataja katika kitabu kitakatifu cha biblia Mika aya ya 8 nayo
ni kutenda haki,kupenda kuwa na rehema na kutembea kwa unyenyekevu mbele
zake,”alisema Ash.
Alisema
kila mkristo, inampasa atafute haki kwa ajili ya watu wenye albinism
maana siku ya mwisho wa maisha ukifika Mungu ndiye atakuwa muendesha
mashtaka na jaji ambapo wale ambao hawakutenda haki kwa kuwauwa na
kuwafanyia ukatili watu wenye albinism watashitakiwa maana kutenda haki
ni agizo la mwenyezi Mungu.
Naye
Mchungaji wa kanisa hilo, Valentine Mbuke alisema binadamu wote
wameumbwa na Mungu hivyo ni wajibu wa kila mmoja kutenda haki hakuna
aliye na haki ya kuwanyima watu wenye albinism au binadamu mwenzie haki
ya kuishi au kuthaminiwa.
0 comments:
Post a Comment