Pages

Ads 468x60px

Friday, June 19, 2015

Mbwa Kichaa Adaiwa Kung’ata Watu 26



WATU  26, wanadaiwa kung’atwa na mbwa anayesadikiwa kuwa na ugonjwa wa kichaa cha mbwa, huku wengine wakijeruhiwa kichwani katika Kijiji cha Iragula wilayani Kilombero.

Hayo yalibainishwa na baadhi ya wananchi  wakati wakizungumza na  jana, ambapo walisema watu  hao waling’atwa wakiwa wanaelekea kwenye shughuli zao za kila siku

Wananchi hao, walisema   watu hao waling'atwa na mbwa wenye ugonjwa wa kichaa Juni 15, mwaka huu.

Kwa upande wake, Ofisa Kilimo Wilaya ya Kilombero, Vicent Mwambirambo  alisema mwananchi aliyenga’twa kichwani  na kusababishiwa majeraha alikimbizwa katika Hospitali ya Mtakatifu Francis kwa matibabu.

Hata hivyo, alisema wanaendesha msako mkali ili  kuwakamata mbwa hao  wasiendelea kuongeza madhara mengi zaidi.

0 comments:

Post a Comment

SHARE