Pages

Ads 468x60px

Friday, June 19, 2015

Polisi Wakamata SMG Na Risasi 110.



JESHI  la Polisi  Mkoa wa Katavi kwa kushirikiana  na askari  wa Hifadhi  ya Taifa (TANAPA) , wamefanikiwa kukamata  bunduki moja   aina ya Sub Machine Gun (SMG)  ikiwa risasi  110 ikiwa umefichwa  katika Kijiji cha  Nzaga  kata ya Ulwira  Wilaya ya Mlele.
 
Kamanda wa  Polisi wa Mkoa wa Katavi,  Dhahiri Kidavashari aliwaambia  waandishi wa  habari jana  kuwa  askari walikamata silaha hiyo  usiku wa kumkia jana
 
Alisema kabla ya tukio hilo,askari wa Hifadhi ya Taifa ya Katavi na polisi  walipata  taarifa  kutoka kwa raia wema  kuwa kuna  mtuhumiwa   mmoja   jina limehifadhiwa ambaye ametoroka  kwa kuwa  bado anatafutwa  kuwa  anajishughulisha  na shughuli  za  ujangili, anamiliki  silaha  moja  ambayo  huitumia kwa shughuli hizo.
 
Alisema baada ya askari hao kufika nyumbani kwa mtuhimwa,  waliizingira  nyumba yake  na ndipo  walipoingia ndani na kukuta mtuhumiwa hayupo.
 
Alisema askari  walifanya upekuzi  na  walifanikiwa kukamata    bunduki  hiyo yenye  namba  C 2136, ikiwa na magazine mbili zikiwa  zimehifadhiwa ndani ya mfuko.

Kamanda Kidavashari,  alisema  pamoja na mtuhumiwa kutoroka  juhudi  za kumtafuta  zinaendelea   pamoja  na   washirika  wanzake

0 comments:

Post a Comment

SHARE