SERIKALI
imesema vijana nchini wenye umri kati ya miaka 10 hadi 24 wanakabiliwa
na janga la taifa la maambukizi ya virusi Ukimwi , mimba za utoto na
vifo vinavyotokea wakati wa kujifungua kitendo ambacho kinadhoofisha
nguvu kazi kazi ya maendeleo ya taifa.
Imesema
vijana ambao ni tegemeo kubwa la taifa lakini wamejiingiza katika
ngono zembe na kuoa au kuolewa wakiwa katika umri mdogo jambo ambalo
limesababisha kundi hilo kuishi na maambukizi ya virusi vya Ukimwi na
vifo wakati wa kujifungua.
Katibu
Tawala wa Mkoa wa Mwanza, Dk. Faisal Issa, alikuwa akizungumza kwenye
ufunguzi wa mkutano wa uhamasishaji juu ya afya ya uzazi na maendeleo ya
vijana.
Alisema vijana walio na umri katia ya miaka 10 hadi 24 wapo katika kipindi cha mabadiliko ya saikolojia na mwili.
Dk.
Issa alisema takwimu za sensa ya 2012 zinaonyesha vijana nchini ni
zaidi ya asilimia 31 ambapo kundi hilo lipo katika hatari ya kukumbwa
na matatizo ya afya ya uzazi, magonjwa ya kuambukizwa kwa nia ya ngono.
“Kiwango
cha vifo vya wanawake vinavyotokana na matatizo ya uzazi kitaifa ni 454
kwa kila vizazi hao 100,000. Mimba katika umri mdogo huchangia mara
mbili hadi tano ya vifo.
“Kwa
Mkoa wa Mwanza akina mama waliohudhuria kliniki ni 131,536 lakini
kati ya hao 27,727 ni vijana wa chini ya umi wa miaka 20 ambao ni
asilimia 21.
“Kiwango
cha vifo vya wanawake vitokanavyo na uzani ni 112 kwa kila vizazi hao
100,000 kwa mwaka 2010 lakini mwaka 2014, vifo 113 vilitokea kati ya
vifo hao 100,000 ambapo kati ya hivyo vifo 40 vilikuwa kwa upande wa
vijana chini ya miaka 24 ambayo ni asiliamia 35,” alisema.
Alisema
kutokana na hali hiyo Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Kitengo cha
Afya ya Uzazi na Mtoto, kimeanzisha semina maalumu ya elimu kwa makundi
hayo ili kubadili tabia na kupunguza maambukizo ya Ukimwi na vifo vya
uzazi.
0 comments:
Post a Comment