WAZIRI
Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye amekionya Chama Cha Mapinduzi (CCM)
kutopitisha mgombea urais kwa njia ya rushwa kwa vile kufanya hiyo
kutawaingiza wapinzani Ikulu.
Sumaye
ambaye ni miongoni wa makada wanaowania kuteuliwa na CCM kugombea
nafasi hiyo, aliyasema hayo juzi mjini Bariadi alipowashukuru wana
CCM 45 waliomdhamini mkoani hapa .
Akizungumza
na baadhi ya viongozi wa chama hicho na wadhamini hao, aliwashukuru
waliomdhamini na kueleza kuwa ikiwa CCM itapitisha wagombea kwa njia za
rushwa utakuwa mwanzo wa vyama vya upinzani kuchukua nchi.
“Nyinyi
kama wajumbe wa NEC mtambue kuwa Tanzania kwa sasa tunahitaji kiongozi
atakayetuvusha, tukichagua kwa rushwa tunawapatia wapinzani nafasi
kuingia Ikulu hivyo chama changu kinapaswa kisipitishe mtu kwa rushwa,”alisema.
Alisema
sababu kubwa itakayofanya wapinzani kuongoza nchi ni rushwa ndani ya
CCM aliyoeleza kuwa imekithiri kwa kiwango kikubwa hasa kwa sasa
kuelekea kipindi cha Uchaguzi Mkuu.
“Sijatoa
rushwa tangu nianze kutafuta wadhamini , watu wanajitolea tu kwa
mapenzi yao kunidhamini sina haja ya kuwanunua watu ninaowapata
nawashukuru kwa maana mapenzi yametoka kwao kunidhamini siyo kwa sababu
fulani, ”alisema.
0 comments:
Post a Comment