Waziri wa Habari Na Michezo Atuma Salamu Za Rambi Rambi Kwa Baraza Kuu La Waislamu Kufuatia Kifo Cha Sheikh Mkuu wa Tanzania
Mpekuzi blog
Waziri
wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mheshimiwa Dkt. Fenella
Mukangara (Mb.) ametuma salamu za rambirambi kwa Baraza Kuu la Waislamu
Nchini (BAKWATA) na Waislamu wote nchini kufuatia kifo cha Sheikh Mkuu
wa Tanzania Mufti Shaaban Issa Bin Simba kilichotokea Jumatatu, tarehe
Juni 15,2015 katika hospitali ya TMJ Jijini Dar es Salaam alipokuwa
anatibiwa.
Katika
salamu hizo, Mhe. Mukangara amesema kuwa ni jambo la kusikitisha
kumpoteza kiongozi huyo ambaye bado Taifa lilikuwa likimuhitaji hasa
katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi Mkuu wa mwezi Oktoba mwaka
huu.
Waziri
huyo ameongeza kuwa Mufti atakumbukwa kwa upole , unyenyekevu wake na
kutopenda makuu,wakati wa uhai wake marehemu alikuwa tayari kumsikiliza
kila mtu bila kujali dini au kabila lake.
“Nimepokea
kwa huzuni nyingi taarifa ya kifo cha Sheikh Mkuu wa Tanzania Mufti
Shaaban Issa Bin Simba ambaye alikuwa Kiongozi anayeshirikiana vizuri na
viongozi wote wa serikali na vyama mbalimbali katika kuhakikisha
Watanzania wanaendelea kuwa wamoja” amesema .
Amesema Waziri Mukangara:
“Nakutumia salamu zangu za rambirambi wewe Katibu Mkuu, BAKWATA na
waislamu wote nchini na naungana nanyi katika kuomboleza msiba huu
mkubwa katika nchi yetu.
"Aidha,
kupitia BAKWATA, natuma salamu za dhati ya moyo wangu kwa familia ya
marehemu kwa kumpoteza mpendwa wao. Napenda wajue kuwa msiba wao ni
msiba wangu. Pia, naungana nao katika kumwomba Mwenyezi Mungu, Mwingi wa
Rehema aiweke pema peponi roho ya marehemu … Amina.”
Imetolewa na;
Idara ya Habari(MAELEZO)
15 Juni,2015
0 comments:
Post a Comment