Omar
Al Bashir, Rais wa Sudan ameripotiwa kuondoka Afrika Kusini pamoja na
kuwepo kwa amri ya mahakama ya nchi hiyo kumzuia kuondoka.
Awali
ndege ya Al Bashir iliripotiwa kuwa ilikuwa imetoweka katika kiwanja
cha ndege Johannesburg na kuhamishiwa katika kiwanja cha jeshi nchini
humo.
Tayari mtandao wa habari wa AFP umeripoti kuwa Rais Bashir ameshatua mjini Khartoum, Sudan.
Walipoulizwa juu ya Bashir, maafisa wa Wizara ya sheria ya Afrika Kusini wamedai kuwa hawajui Rais huyo alipo.
Mapema
leo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon alikuwa amesistiza
kuwa amri ya mahakama ya Uhalifu ya Kimataifa, ICC lazima iheshimiwe na
Afrika Kusini.
Ndege
inayosadikiwa kuwa ya Rais Omar Bashir wa Sudan ikiruka kutoka uwanja
mmoja wa ndege karibu na mji wa Preatoria, nchini Afrika Kusini
Kuondoka kwa Bashir kumekuja kabla ya uamuzi rasmi wa mahakama wa kama akamatwe au la.
0 comments:
Post a Comment