WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais (Kazi Maalumu), Profesa Mark Mwandosya amerejesha fomu zake za kuwania kupeperusha bendera ya CCM katika nafasi ya urais.
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuwasilisha fomu yake
alisema akichaguliwa kuwa rais atahakikisha kuwa na utawala bora,
kuboresha huduma za jamii na kuhakikisha amani na usalama wa nchi
unadumishwa.
Profesa Mwandosya ambaye amekuwa mgombea wa 12 kurejesha fomu ambayo
ilipokelewa na katibu wa oganaizesheni, Mohamed Seif Khatib, alisema pia
kwamba amefurahishwa na wagombea wenzake ambao amesema kwamba
watamuunga mkono.
Mpaka juzi wanachama 40 wa CCM amechukua fomu kuwania kuteuliwa kuwa
mgombea wa CCM katika kinyang’anyiro cha Urais katika uchaguzi mkuu ujao
unaotarajiwa kufanyika Oktoba.
Tarehe ya mwisho ya urejeshaji wa fomu ni Julai 2. Profesa Mwandosya
amesema kwamba amefurahishwa sana na kauli za wagombea wenzake kwamba
watamuunga mkono kama atapitishwa na CCM kuwa mgombea.
Aidha amesema kwamba anamshauri mgombea mwenzake wa nafasi hiyo,
waziri mkuu wa zamani Edward Lowassa kufanya kama hao wengine ili
kurahisisha kazi ya CCM kupata mgombea wake katika nafasi ya Urais.
Alisema kwamba ametembea katika mikoa 31 katika harakati za kutafuta
wadhamini na kuwapongeza viongozi wa chama chake katika wilaya kwa
kufanikisha uratibu uliowezesha wagombea kupata wadhamini.
“Hata hivyo nimewasilisha udhamini kutoka mikoa 12 ya Bara na mitatu
ya Zanzibar zikiwa na wadhamini 30 kwa kila mkoa na kufanya jumla ya
wadhamini kuwa 450 wanaotakiwa na chama,” alisema Profesa Mwandosya.
Aliitaja mikoa hiyo kuwa Dodoma, Morogoro, Pwani, Dar es Salaam,
Mjini Unguja, Unguja Kusini, Unguja Magharibi, Pemba Kusini, Pemba
Kasikazini, Tanga, Mwanza, Geita, Kagera, Shinyanga, Simiyu, Mara,
Songea, Njombe, Iringa, Tabora, Kigoma, Katavi, Rukwa na Mbeya.
0 comments:
Post a Comment