Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ amejikuta akiangua kilio bungeni baada ya kutoa hoja binafsi kumjibu Mbunge wa viti maalum wa Singida ‘CCM’ Martha Mlata, aliyemshutumu kwa kumpora mtoto wake wa kike Sasha kutoka kwa mzazi mwenzake Faiza Ally.
Akijibu tuhuma za Mlata, Sugu alisema kuwa ameumizwa na kusitikishwa
kwa suala la kifamilia kuingizwa ndani ya bunge na kuomba kuheshimiwa
kwa kuwa masuala yale ni masuala binafsi.
“Asante sana Naibu Spika, naomba nitoe
maelezo binafsi, tarehe 25 June 2015, Mbunge Martha Mlata alidai
kuwa kuna Mbunge wa CHADEMA amempora mwanamke mmoja mtoto mdogo wa miaka
miwili na amempora wakati Mbunge huyo amekuwa hatoi matunzo kwa mama
yake… Mlata aliwataka Wabunge wote wanawake kuungana kukemea kitendo
alichodai kimefanywa na Mbunge huyo," Alisema Sugu na Kuongeza:
“Hakutaja jina la Mbunge aliyemhusisha na madai yake ila alidai kuwa
ni msanii mwenzake… hata hivyo alitaja jina la mwanamke anayedaiwa
kunyang’anywa mtoto kuwa ni Faiza. Mbunge aliyelengwa na mashambulizi ni
mimi Joseph Osmond Mbilinyi, mimi ndiye baba wa mtoto Sasha Desderia
Mbilinyi anaedaiwa kuporwa kwa mama yake, na Faiza aliyetajwa ni Faiza
Abdallah Ally ambaye ni mzazi mwenzangu na mama mzazi wa Sasha Desderia.
“Watu wazima hawapendelei kuzungumzia mambo binafsi hadharani…
Nadhani sitakosea kusema hata Mheshimiwa Martha mwenyewe asingependa
kuzungumzia matatizo yaliyopelekea ndoa yake kuvunjika.
“Mimi ni mmoja wa watu wazima wenye akili timamu ndio maana
sijazungumzia hadharani kuhusu uhusiano wangu na mzazi mwenzangu Faiza
Ally na mtoto wetu Sasha… Sasha ameishi na mama yake tangu alipozaliwa
mwaka 2012, katika kipindi chote nimempelekea mama yake laki tano kila
mwezi, nimemlipia ada ya shule Milioni 3 kila mwaka.. Mlata kama
angekuwa anataka kujua angeniuliza ningempatia taarifa hizi kabla
hajarusha tuhuma nzito.
“Mwanamke anayedaiwa kuwa mnyonge anajulikana katika kumbi za starehe
nchi nzima, picha zake zilisambazwa katika Mitandao ya Kijamii na
kuleta fedheha kubwa kwa watu wanaojali maadili ya mavazi, picha zake
nyingine akiwa amevaa diapers zilisambaa mitandaoni na Martha Mlata
angeweza kupata ukweli wa mambo haya kabla hajarusha tuhuma mbele ya
Bunge.
“Nilienda Mahakama ya Mwanzo Manzese, niliwasilisha ushahidi kwamba
mzazi mwenzangu asingeweza kumlea mtoto.. Mahakama ilimwita akajitetea,
June 23 Mahakama iliridhika na ushahidi wangu, ikaamua mtoto akabidhiwe
kwangu ili nimlee.
"Kilichodaiwa kuwa ni uporaji wa mtoto kiukweli ni amri ya Mahakama, Mlata hakuwahi kuonekana Mahakamani, nina mashaka hata kama anamfahamu mtoto mwenyewe au mama anayemwita mwanamke mnyonge“
"Kilichodaiwa kuwa ni uporaji wa mtoto kiukweli ni amri ya Mahakama, Mlata hakuwahi kuonekana Mahakamani, nina mashaka hata kama anamfahamu mtoto mwenyewe au mama anayemwita mwanamke mnyonge“
"Pamoja na Mahakama kunipa haki, mtoto bado yuko kwa mama yake kwa sababu mimi ni mstaarabu… nimetoa nafasi ili Majadiliano ya kifamilia yafanyike… Naomba mjadala huu usiendelee zaidi ya hapa”.
Baada ya maelezo hayo, Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai alisimama na kuomba mjadala huo ufungwe ili kulinda haki za mtoto.
0 comments:
Post a Comment