Zoezi la uandikishaji wa wapigakura kwa kutumia mfumo mpya wa kielektroniki (BVR) mkoani Mwanza linaigia siku ya tatu huku kasi ndogo ya uandikishaji ikishuhudiwa katika baadhi ya vituo vya kuandikishia wapiga kura kutokana na uhaba wa vifaa pamoja na wataalam, hali ambayo imelalamikiwa na baadhi ya wakazi wa kata za wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza.
Kufuatia
hali hiyo baadhi ya wakazi wa mkoa wa Mwanza wameiomba tume ya taifa ya
uchaguzi NEC kuongeza idadi ya mashine za BVR pamoja na waandikishaji
wenye ujuzi wa kuzitumia mashine hizo.
Mkoa
wa Mwanza umepewa mashine 571 za BVR ambazo zitatumika kuandikisha
wapiga kura zaidi ya milioni moja na laki nne katika vituo 1500 vya mkoa
huo.
0 comments:
Post a Comment