Mgombea
urais kupitia CCM, Dk. John Magufuli, anatarajiwa kuwahutubia wakazi
wa Mkoa wa Mwanza keshokutwa ikiwa ni sehemu ya kujitambulisha.
Akizungumza
jana na waandishi wa habari jana, Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza, Miraji
Mtaturu, alisema Dk. Magufuli atawasili Mwanza siku hiyo mchana na
kwenda moja kwa moja kwenye Uwanja wa Furahisha.
Alisema
Dk. Magufuli atapokewa na viongozi mbalimbali wakiwamo wa dini, siasa
na Serikali na aliwataka wananchi kujitokeza kumsikiliza mgombea wao.
“Ni
zamu ya Mkoa wa Mwanza baada ya mgombea huyo kutambulishwa mikoa ya
Dodoma, Dar es Salaam na Zanzibar. Baada ya kutoka Mwanza atakwenda
mkoani kwake Geita."
Alisema
kutokana na umaarufu wa Dk. Magufuli ambaye aliwahi kufanya kazi
Mwanza, aliwaomba wananchi wote kufika wakiwamo mama lishe, waendesha
pikipiki, wanafunzi wa sekondari na vyuo vikuu vilivyopo jijini .
Mtaturu alizungumzia kauli ya hivi majuzi ya mwanasiasa mkongwe, Kingunge Ngombale-Mwiru na kusema:
“Nimeshangazwa
na kauli iliyotolewa na Kada wa chama chetu, Kingunge Ngombale Mwiru
ya kushambulia Baraza la Wazee wastaafu ambao ni viongozi wetu wa chama
na Serikali, akiwatuhumu kuendesha vikao vya mchakato wa kumpata mgombea
urais kwa mizengwe na ajenda zao za siri.
“Mzee
huyu aliaminika na kusifika akiwa mwalimu mzuri wa siasa aliyefundisha
somo hilo Chuo cha Kivukoni akisisitiza chama kwanza mtu badaye,
sasa tunashangaa leo anageuka na kufikiria kwa tumbo badala ya akili.”
“Anajivunjia
heshima yake inawezekana amesahau ibara ya 29 ya katiba ya CCM
inayotambua wazee. Hatukutarajia mzee atasema maneno hayo baada ya
mgombea urais wa chama kupatikana…basi angesema awali kwa kushauri,” alisema.
Maturu
aliwataka waliokuwa wagombea urais kuvunja makundi yao na kumuunga
mkono mgombea wa chama hicho kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba.
0 comments:
Post a Comment