Kundi la Wakenya, limejiapiza kumkaribisha rais wa Marekani, Barack
Obama, nchini kwao wakiwa hawajavaa nguo ili kuonesha kuwa
hawajakubaliana na kitendo cha kuruhusu mapenzi ya jinsia moja.
Obama anatarajiwa kutembelea Kenya kwa mara ya kwanza tangu kuwa
rais na kutegemea kuwa na mkutano na wafanyabiashara kuanzia Julai 24-26
mwaka huu.
Kwa mujibu wa barua iliyosambazwa na kundi hilo la wakenya, imedai
kuwa watafanya maandamano ya amani jijini Nairobi, Julai 22 na 23 mwaka
huu kuanzia Uhuru kona.
Wamedai kuwa maandamano hayo yatafanywa na wanawake pia wanaume
takriban 5,000 wakiwa watupu bila nguo yoyote kupinga Umoja wa nchi za
Amerika kupitisha sheria ya mashoga kutambuliwa kisheria.
Wamesema lengo kuu la maandamano wakiwa uchi ni kumuonesha na
kuelewesha rais Obama, utofauti uliopo kati ya wanawake na wanaume.
Wiki iliyopita, Wakenya hao walienda katika mitaa kuandamana
wakimuonya rais Obama, kutothubutu kuzungumzia suala la haki za mashoga
kwenye ziara yake ya kutembelea nchi hiyo.
Mbunge Charles Njagagua, pia aliwataka wabunge kumfukuza Obama, nje ya Bunge mara moja akigusia haki za mashoga.
Naye Makamu wa rais nchini Kenya, William Ruto, hivi karibuni
alinukuliwa na vyombo vya habari akiwaambia wananchi wake kuwa wamesikia
kuwa Marekani wameruhusu uhusiano wa mashoga na mambo mengine yasiyo na
maadili na kuwataka viongozi wa dini kutetea nchi yao na kusimamia
imani ya nchi yao.
0 comments:
Post a Comment