Sakata la Mwanamuziki Shilole kucheza huku baadhi ya sehemu za
matiti zikiwa wazi limechukua sura mpya Bungeni leo kufuatia Naibu
Waziri wa Habari vijana na Utamaduni na Michezo Juma Nkamia kutangaza
kuwa inasubiria uamuzi wa Baraza la sanaa Taifa (Basata).
Aidha, Nkamia amesema suala la shilole hivisasa lipo chini ya
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) ambapo mara baada ya kumaliza
mahojiano naye litapelekwa wizara ya habari vijana na utamaduni na
michezo kwa hatua nyingine zaidi.
Hivi karibuni Shilole aliwaomba msamaha watanzania kwa madai kuwa anajutia kutozingatia
maadili katika onesho hilo lililofanyika nchini Ubelgiji na kuzua gumzo
nchini Tanzania.
0 comments:
Post a Comment