WAKATI
Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa akitarajiwa kesho kutangaza nia
yake ya kugombea urais mjini Arusha katika Uchaguzi Mkuu mwaka huu,
Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Steven Wassira amepanga
kutangaza safari yake ya kuelekea Ikulu Jumapili, jijini Mwanza.
Wassira
mwenye Shahada ya Uzamili katika Uchumi ambaye pia ni Mbunge wa Bunda
mkoani Mara, anakusudia kutangaza nia yake hiyo ya kugombea urais
kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika ukumbi wa Benki Kuu ya
Tanzania (BoT).
Taarifa
za kuaminika zilizoifikia Mpekuzi kutoka kwa watu wa karibu na
Waziri Wassira zinaeleza kuwa pia atatangaza siku ya kwenda
kuchukuwa fomu ya kuwania nafasi hiyo kwenye Ofisi za Makao Makuu ya CCM
mjini Dodoma.
“Ni
kweli tarehe 31 mwezi huu 2015 siku ya Jumapili, Waziri Steven Wassira
atatangaza kusudio lake la kugombea urais katika Uchaguzi Mkuu mwaka
huu kupitia CCM. Nia yake hiyo ataitangazia Mwanza katika ukumbi wa
BoT.
“Mzee
(Wassira) anahitaji kuwatumikia Watanzania kwa dhamira njema ya kuleta
mabadiliko chanya ya kimaendeleo dhidi ya wananchi. Yapo mambo mengi
atayaeleza siku hiyo pamoja na tarehe rasmi ya kuchukua fomu,” alisema mtoa habari huyo aliyepo karibu na Waziri Wassira.
Wassira
alizaliwa mwaka 1945 Wilaya ya Bunda mkoani Mara, alisoma Shule ya
Msingi ya Balili na Kisangwa Middle School, Wilaya hiyo ya Bunda,
baadaye alijiunga na masomo yake ya Sekondari katika Shule ya British
Tutorial College.
Alipata
masomo ya ngazi ya juu Marekani katika Shahada tatu za Uchumi na
Utawala, Shahada ya kwanza ya Uchumi na Uhusiano wa Kimataifa, Shahada
ya Uzamili ya Uchumi na Shada ya Uzamili katika Utawala, zote kutoka
Chuo Kikuu cha Amerika (American University) Jijini Washngton D.C.
Mbali
na kuwa mbunge kuanzia mwaka 1970, Waziri Wassira amekuwa mtumishi wa
umma kwa muda mrefu serikalini, ambapo alipata kuteuliwa na Mwalimu
Julius Kambarage Nyerere, kuwa Naibu Waziri wa Kilimo.
Mwaka
1975 Mwalimu Nyerere alimteua kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara, nafasi
aliyoitumikia hadi 1982 alipoteuliwa kuwa Waziri na Ofisa Mwandamizi
katika Ubalozi wa Tanzania Washington D.C Marekani.
Nyadhifa
nyingine alizowahi kuzishika Wassira ni Naibu Waziri wa Serikali za
Mitaa, Waziri wa Kilimo na Maendeleo ya Mifugo mwaka 1989 hadi 1990,
Waziri wa Maji, Waziri Ofisi ya Rais (Uratibu na Uhusiano), Waziri wa
Chakula, Kilimo na Ushirika nafasi aliyonayo sasa.
0 comments:
Post a Comment