MTU mmoja
aliyetambuliwa kwa jina la Juma Mwinyivue maarufu kama ‘Tabambwa’ (28)
mkazi wa Zogowale, Visiga mkoani Pwani, alijikuta katika wakati mgumu
baada ya mwanamke aliyetarajia kumuoa, aliyetajwa kwa jina moja la Manka
(20) kumzimia simu na kuingia mitini siku chache kabla ya ndoa yao,
tukio lililotokea Mei 23, mwaka huu.
Juma Mwinyivue maarufu kama ‘Tabambwa' anayedaiwa kutorokwa na mchumbaake.
Kwa
mujibu wa mpambe wa bwana harusi, Saidi Matakope, ndugu na marafiki wa
bibi harusi walitayarisha ngoma maarufu ya Kigodoro na vyakula wakiamini
binti yao atapata mume, lakini hadi ilipofika jioni, mwanaume hakuweza
kutokea na kuwaacha watu vinywa wazi.
Katika eneo la tukio, mume mtarajiwa Juma, alisema alikutana na Manka na kumchumbia mwanzoni mwa Machi.
Baada
ya kuridhika na kukubaliana, ndoa ilipangwa kufanyika Mei 23, mwaka huu
huku akiwa tayari ameshalipa mahari na kila kitu cha muhimu.
Lakini
wiki mbili kabla ya ndoa, Juma alidai kutompata mke wake hewani baada
ya kukubaliana kwenda kurekebisha shela la harusi, kitu kilichomshangaza
kwani hata alipofika nyumbani kwake, alikuta mlango wa nyumba yake
ukiwa umefungwa.
Juma alisema kuwa alipompigia simu yake ilikuwa haipatikani na kuamua kwenda kwa mama yake mzazi ambaye naye hakuwa akijua mwanaye ameelekea wapi huku siku zikiwa ukingoni.
Manka anayedaiwa kukimbia ndoa.
“Siku
iliyofuata nikampigia mama yake akaniambia mwanaye ameelekea Iringa kwa
shangazi yake. Nikashangaa na kuuliza kwa nini hakuniaga. Nilimpigia
simu yake ikawa inaita, inakata au kutopatikana kabisa. Kwa hivyo
nikamwambia mama mkwe kwamba mwanaye sitamuoa tena na nimesamehe gharama
zote nilizotoa,” alisema Juma.
Mshenga
wa Juma aliyejitambulisha kwa jina la Kindala, alidai baada ya
kumtaarifu mama Manka kuwa ndoa hakuna, alishangaa baada ya wiki moja
kupigiwa simu na ndugu zake aliulizwa muda ambao mwanaume angeenda kuoa.
“Ndipo tukashangaa na kuwaambia mbona tayari tumeshatoa taarifa kwa mama mtu kwamba hatuoi tena,” alisema mshenga huyo.
Kwa
upande wake, bibi harusi alikiri kusafiri Iringa na shangazi yake, kwa
kile alichodai ni kufanyiwa tambiko la ndoa, lakini akaogopa kumuaga
mwenzake akijua wazi asingekubaliwa. “Bado nampenda na naitaka ndoa hata
kesho nipo tayari, nilikwenda kwa shangazi Iringa siyo kwenye
michepuko,” alisema Manka.
Na Deogratius mongela-GPL
0 comments:
Post a Comment